29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Hassan Rehani awajibu walioikimbia Twanga Pepeta

dogoNA MWALI IBRAHIM

BAADA ya baadhi ya wanamuziki wa bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Ramadhani Athumani na Salehe Kupaza kueleza sababu iliyowafanya waikimbie bendi hiyo na kuhamia Double M Sound Plus ni maslai na madeni yao wanayoidai Twanga Pepeta, meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, ameibuka na kukana madai hayo.

Wanamuziki hao tayari wameshatambulishwa rasmi kwenye bendi ya Double M Sound Plus iliyopo chini ya Mwinjuma Muumini ‘Kocha wa Dunia’, wamedaiwa kutumia maneno ya kudai kama njia ya kuikacha Twanga Pepeta, lakini hawadai chochote kwa kuwa hawakuwa na mkataba na bendi hiyo.

“Wazaramo wana msemo wao kuwa ukitaka kumuua paka inabidi umpe sifa mbaya kwanza na ndivyo walivyofanya wao, lakini hawatudai chochote na mambo mengine yao hatuwezi kuyaweka kwenye vyombo vya habari kwa kuwa hawakuwa na mikataba na bendi hiyo zaidi ya kuwa na makubaliano ya binafsi,” alisema Rehani.

Awali wanamuziki hao waliondoka Twanga Pepeta kwa ruhusa ya mwajiri wao kwa lengo la kuiongezea nguvu, Double M ilipokuwa kwenye ziara ya kimataifa nchini Msumbiji, lakini badala ya kurudi bendi waliyotoka wakaamua kujiunga na bendi hiyo.

Dogo Rama alisema malipo ya mshahara ya miezi nane anayoidai bendi ya Twanga yamemsababishia kuonekana mbaya na uongozi kuamua kumsimamisha, ndiyo sababu ya yake kuondoka katika bendi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles