27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hasara yazikumba timu Ligi Kuu Zanzibar

Okoa.jpg1NA MOHAMED MHARIZO, DAR ES SALAAM

TIMU zinazoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar, zimelalamikia hasara za kiuendeshaji zinazopata kutokana na ligi hiyo kusimamishwa kwa amri ya mahakama kutokana na Chama cha Mpira wa Miguu visiwani humo (ZFA), kukabiliwa na kesi mbalimbali.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kwa simu kutoka Zanzibar, mmoja wa makocha wa timu za Ligi Kuu ya Zanzibar, Ali Bushiriki ambaye ni kocha mkuu wa timu ya KMKM, alisemakwa sasa hawajui hatima ya ligi hiyo kutokana na kesi hizo.

“Kwa suala la uendeshaji timu zinaumia, ukiangalia hadi kufikia hapo ligi itakapoanza na hasa kipindi hiki ambacho hakuna udhamini.

“Ushauri wangu kwa wadau wa soka hasa wanaoongoza mchezo huu sio tu ZFA (Chama cha Soka Zanzibar), bali nchi nzima ya Tanzania, wasilinganishe masuala ya michezo na mambo ya siasa.

“Lakini pia wanaoongoza mpira katika nchi yetu wawe makini na utendaji wao wa kazi, wafuate kanuni na taratibu, matokeo yakewatu wengine au klabu wakiona mambo yanaenda kinyume ndio kama hivi wanaenda mahakamani.

“Ikumbukwe Shirikisho ya Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka ulimwenguni (FIFA), yanakataza masuala ya mpira kupelekwa mahakamani badala yake viundwe vyombo maalumu vya haki kama huko TFF kuna kamati ya nidhamu, kamati ya maadili, sasa huku kwetu kamati za namna hiyo hazipo ndiyo maana haya yanatokea,” alisema.

Hatima ya soka la Zanzibar lipo mikononi mwa mahakama ambapo ZFA inakabiliwa na kesi mbalimbali.

Moja ya kesi hizo ni ile iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Vuga na Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Haji Ameir Haji, inayowakabili viongozi wa juu wa chama hicho, akiwemo Rais wa ZFA, Ravia Idarous Faina, Makamu wa Rais ZFA Pemba, Ali Mohamed Ali na Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Haji Salum.

Haji alifungua kesi hiyo akidai kukiukwa kwa utaratibu wa kuifanyia marekebisho katiba ya chama hicho, kukiukwa kwa taratibu za matumizi ya fedha na kuwepo kwa ubaguzi katika uongozi wa chama hicho.

Kesi nyingine ni ile iliyofunguliwa Agosti 20 mwaka huu na timu ya Chuoni katika Mahakama ya Mjini, ikipinga kushushwa Daraja la Kwanza, hivyo kusababisha mahakama hiyo kusimamisha Ligi Kuu iliyokuwa ianze Septemba 20 mwaka huu.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles