Harusi ya Lulu yanukia

0
2156

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM


MWIGIZAJI wa filamu za Bongo Movie nchini Tanzania, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amevishwa pete ya uchumba na mchumba wake wa muda mrefu ambaye ni meneja na mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Majizo.

Tukio la kuvishwa pete kwa mwanadada huyo lilifanyika juzi usiku jijini hapa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Majizo aliandika kuwa mchumba wake huyo amekubali ombi lake la kutaka kufunga naye ndoa.

Lulu na Majizo wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, licha ya kipindi cha nyuma kufanya siri na kukana kutaka kufunga ndoa.

Wawili hao walikuwa wakishindwa kuweka hadharani uhusiano wao, huku wakiamua kuufanya siri kubwa kwa lengo la kukwepa maneno ya mashabiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here