30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Harmonize, Marioo wajifungia studio

Jessca Nangawe

MASTAA wawili wanaofanya vyema kwa sasa kwenye muziki wa bogo fleva, Omary Mwanga ‘Marioo’ pamoja na Harmonize wameingia studio kuandaa ngoma yao mpya.

Akizungumza Marioo alisema moja ya ndoto zake kubwa ni kufanya kazi na msanii mkubwa kama Harmonize na anashukuru kuona ndoto yake inatimia hivi karibuni.

“Ni kweli tupo jikoni, kuna kazi mpya tunaiandaa, lakini ni mapema sana kusema inaitwaje ila mashabiki wakae tayari hii sio yakukosa,”alisema Marioo.

Hata hivyo staa huyo ambaye anafanya vizuri na kibao chake cha Raha, alisema haikuwa rahisi kumpata Harmonize kutokana na kutingwa na shugfhuli zake za muziki hasa ujio wa albamu yake mpya ya AfroEast.

Harmonize yupo kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya albamu yake ya AfroEast inayotarajiwa kuachiwa Machi 14 kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles