28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

HARMONIZE KUFANYA KAZI NA TYGA

NA JESSCA NANGAWE


STAA kutoka lebo ya WCB, Rajab Abdul maarufu ‘Harmonize’, amemtaja staa wa Marekani, Michael  Stevenson ‘Tyga’ kuwa ni mmoja wa wasanii wakubwa anaofikiria kufanya naye kazi mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana,  Harmonize alisema tayari ameanza kufanya mazungumzo ya awali na Tyga ili kufikia makubaliano ya kuweza kufanya kazi pamoja.

“Wapo wasanii wengi, miongoni mwao nafikiria sana kufanya kazi na Tyga, mipango yetu ipo jikoni na wakati wowote mtapata mambo mazuri kutoka kwetu, huu ni mwaka wangu wa kuhakikisha natimiza sehemu ya ndoto zangu ili kuinua muziki wangu uwe wa kimataifa,”     alisema Harmonize.

Kwa sasa staa huyo anafanya vyema na ngoma yake ya ‘Shulala’ akiwa kamshirikisha staa wa Nigeria, Korede Bello.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles