Harmonize aendelea kutesa USA

0
1736

NA JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM


MSANII Rajab maarufu kama Harmonize, yupo nchini Marekani akiendelea kufanya shoo katika miji mbalimbali nchini humo.

Meneja wa msanii huyo, Joel Puaz, aliliambia MTANZANIA kuwa walitua nchini Marekani tangu Alhamisi iliyopita na mwishoni mwa wiki walikuwa wakifanya shoo katika Jiji la Dallas kabla ya juzi Jumapili  kupiga shoo katika Mji wa Hauton nchini Marekani.

“Tunashukuru tumefika salama na tayari tumeanza ziara yetu, tayari tumemaliza miji miwili na tutaendelea tena na ziara yetu katika miji ya Oakland, Seatle, Atlanta, Los Angeles na Washington DC.

Alisema anaamini ziara hiyo itazaa matunda mengi kwani tayari wameendelea kupata mialiko kutoka kwa Watanzania wengi waliopo nchini humo ambayo haikuwa kwenye ratiba zao.

Alisema mara baada ya ziara hiyo, watarejea nchini na kuendelea na ratiba nyingine kwani wamekuwa na ratiba nyingi kuelekea kipindi hiki cha kufunga mwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here