23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

HARMINIZE, WOLPER… SI MSEME TU MAZEE!

Na CHRISTOPHER MSEKENA

SIJAFAHAMU kwanini wapenzi waliowahi kuonyeshana mapenzi wakiachana hugeuka maadui wakubwa na wakati mwingine chuki zao huzionyesha wazi.

Kwa upande wa mastaa wa Kibongo tuliona kwa Diamond Platnumz na Wema Sepetu, Shilole na Nuh Mziwanda au Nuh na mzazi mwezake Nawali na Gadner na Lady Jay Dee.

Kapo nyingine ni Barnaba na Mama Steve na wengine wengi ambao hata wewe unaweza kuwakumbuka. Hata hivyo, wapo wengine walishazimaliza tofauti zao na sasa wapo poa.

Uadui na chuki za wazi zimeonekana wiki hii kwa waliowahi kuwa wapenzi, msanii wa Bongo Fleva, Harmonize na mwigizaji Jacqline Wolper kutupiana maneno yaliyoonyesha kuwa mbali na kuachana kwao kila mmoja ana hasira juu ya mwenzake.

Inafahamika hivi sasa Wolper yupo kwenye penzi zito na kijana anayeitwa Brown huku Harmonize akijivinjari kwenye dimbwi la mahaba na mrembo wa Kizungu anayeitwa Sarah.

Kila mmoja kwa nafasi yake amekuwa akila bata na mpenzi wake sehemu tofauti tofauti duniani huku akionyesha kuwa na furaha zaidi kuliko hapo awali jambo linaloonyesha wanakomoana kwa lengo la kuumizana.

Gumzo la Town wiki hii lipo na wimbo wa ziada (Bonus Track) ambayo Harmonize ameiachia kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki zake. Wimbo huo unaitwa Nimechoka ambayo ndani yake kuna mistari iliyogusa hisia za X wake (Jacqueline Wolper).

Baadhi ya mistari kwenye wimbo huo wa ziada inasema: Kila chenye marefu na mapana, huwaga hakikosi mwisho, yanini kulumbana kukicha bila suluhisho, kwenye kisicho riziki hakiliki sasa yanini tutoane roho, nimepungukiwa nini, mbona naishi sija hata haja jiba la roho, na ule utundu wa mapenzi kushindana mimi na wewe.

Niliuvumilia na siyo kama siwezi kupata aliyezaidi ya wewe, ila hii dunia na ninajichunga sana.

Mistari hiyo iligusa hisia za Wolper na kuhisi kama Konde Boy anamkosea adabu ndipo naye akatumia ukurasa wake wa Instagram na kumjibu Harmonize na kuandika:

“Unanitungia nyimbo halafu unasema ooo hunifikirii, mtu mpaka unaingia studio unaimba mipasho yako si inamaana nimekujaa kwenye koo, mpaka mwili yaani mpaka tukikupima group lako la damu tunaweza kupata WOLPER MASSAWE.

“Sikiliza nimelala chini, nimekufumania, nimekuta meseji za wanaokutafutia wanawake lakini sijawahi kuongea kwa sababu najua nini maana ya mahusiano, kuna kuachana.”

Harmonize amejitetea kwa kusema ni kawaida yake kuimba nyimbo zinazoigusa jamii kama alivyofanya katika ngoma yake ya Sina ambayo ilikuwa inamwelezea mtu aliyekuwa na mafanikio na baadaye akafulia ambao kwenye kichupa alionekana msanii Mr Nice.

Hivyo hivyo katika Bonus Track hiyo alikuwa anaelezea vitu ambavyo vinatokea kwenye jamii na havihusiani kabisa na Wolper kwani hivi sasa hamfikirii tena na majeshi yake yapo kwa mpenzi wake mpya mwenye mkwanja mrefu, Sarah.

Nani anayejua ukweli? Ni wao wenyewe – Harminize na Wolper. Siye yetu macho.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles