26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Harakati za Marekani zahofiwa Taiwan

SINGAPORE CITY, SINGAPORE 

OFISA Mkuu wa Jeshi la China, Shao Yuanming amesema harakati za Marekani nchini Taiwan na Bahari ya Kusini ya China haziwezi kuwa na utulivu katika ukanda huo.

Yuanming alitoa kauli hiyo jana akijibu maoni ya Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Patrick Shanahan aliyedai kuwa China imekuwa ikidhoofisha uw2epo wa amani katika ukanda huo.

“Yeye (Shanahan) amekuwa akielezea maoni yasiyo sahihi na kurudia sauti za zamani kuhusu masuala ya Taiwan na Bahari ya Kusini ya China,” alisema Yuanming kuwaambia waandishi wa habari baada ya hotuba ya Shanahan.

“Hii inaathiri amani na utulivu wa kikanda,” aliongeza.

Yuanming aliongeza kuwa China itaweza kulinda uhuru wake kwa gharama yoyote dhidi ya yeyote anayejaribu kuitenga Taiwan kutoka eneo lake. 

“China itabidi kuunganishwa tena, ikiwa mtu yeyote anataka kuitenganisha Taiwan kutoka China, jeshi la China litalinda uhuru wa nchi kwa gharama zote,” alisema. 

Mapema, Shanahan aliwaambia wajumbe katika jukwaa la utetezi huko Singapore kwamba Marekani haitanyamaza tena juu ya tabia ya China barani Asia, huku kukiwa na tishio la kukosekana utulivu katika eneo hilo kuanzia Bahari ya Kusini ya China hadi Taiwan.

Shanahan aliitaja China kama taifa linaloharibu hali ya hewa katika ukanda huo.

Hata hivyo, Yuanming alijibu mapigo akisema kwamba Marekani ndiyo inayoodhoofisha hali ya utulivu katika ukanda huo kutokana na hatua zake za hivi karibuni.

Mei mwaka huu, meli ya kivita ya Marekani ilitia nanga karibu na kisiwa cha Scarborough Shoal katika Bahari ya Kusini ya China, ikichukizwa na Beijing wakati wa mvutano wa kibiashara kati ya mataifa hayo makubwa kiuchumi duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles