25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Hapi apiga marufuku michango ya fedha shuleni, aruhusu ya chakula

Francis Godwin – Iringa 

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, amepiga marufuku michango ya fedha za chakula kwa wazazi wa shule zote za mkoa huo na kwamba wazazi wanapaswa kuchangia chakula sio pesa.

HAPI alitoa agizo hilo jana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Luganga wilayani Kilolo baada ya wazazi kulalamikia michango ya Sh 150,000 ambayo wanatakiwa kupeleka shuleni kwa ajili ya chakula cha watoto wao .

Hapi alisema lengo la Serikali  ni kufuta michango katika shule za sekondari na msingi ili watoto wote waende shule.

Hivyo alisema si sahihi kuwatoza wazazi fedha za chakula badala yake wazazi kupitia utaratibu ambao utawekwa na kamati za shule, wachangie chakula na sio pesa .

“Wekeni bajeti ya chakula kwa wanafunzi shuleni kama ni kila mwanafunzi ni kuchangia debe la mahindi na maharage kwa mwaka, kila mmoja achangie chakula sitaki kusikia michango ya fedha,” alisema Hapi 

Alisema mazao hayo yakikusanywa, itakuwa jukumu la shule kusaga mahindi kwaajili ya chakula.

Alisema baadhi ya walimu na kamati za shule zimegeuza wazazi ni mtaji kwa kuwatoza michango isiyo na risti ambayo ni kero kwa wazazi .

Alisema suala la chakula kwa watoto ni muhimu na mkoa unahimiza watoto kupata chakula ila utaratibu wa chakula usiwe kero kwa wazazi.

Hapi alisema walimu wakuu wote wanapaswa kuzingatia maagizo hayo na wale watakaokwenda kinyume na watachukuliwa hatua.

Awali baadhi ya wananchi wa walidai baadhi ya shule zimekuwa zikiwatoza fedha za chakula Sh 150,000 tena bila ya kupewa risti yoyote .

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles