23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Hapi aiagiza TRA kuwasaka wanaokopesha fedha kwa riba

FRANCIS GODWIN, IRINGA

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ali Hapi,  ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa, kuwasaka na  kuwabana watu wote wanaojihusisha na  biashara ya kukopesha fedha zenye riba  kubwa kwa wananchi.

Agizo hilo alilitoa mjini hapa jana wakati wa ziara yake ya kupokea na kutatua  migogoro ya ardhi wilayani Mufindi.

Alisema watu hao waliokuwa wakikopesha  fedha za riba kwa wananchi wamekuwa ni chanzo kikubwa cha wakazi wa Iringa  kupoteza mali zao walizoziwekeza kama dhamana ilhali hawalipi kodi TRA.

“Kwa hiyo madudu yapo mengi na saa nyingine mnatuona tunakuwa wakali ila  wapo watu wengine wanaojiita haki za  binadamu wamekaa Dar es Salaam katika  kiyoyozi wanapiga kelele hawajui huku  wananchi wanavyonyanyasika kiasi gani na watu wamepoteza ndugu zao kwa kufa kwa presha kutokana na mali zao kupokonywa na hawa wakopeshaji ila yote haya wao hawayaoni wapo kunilalamikia mimi ninayesaidia wanyonge,” alisema.

Alisema hatawasikiliza wachache  wanaotetea unyonyaji na badala yake atawasikiliza wananchi walio wengi.

“Wakati mwingine Serikali inaharibiwa na watendaji ambao wameacha kutimiza  wajibu wao wa kuwasikiliza wananchi na  kutenda haki, mimi sihitaji kabisa  kupendwa na wachache wanaotapeli haki za wananchi, nahitaji kupendwa na  wanyonge walio wengi ambao kazi yangu ni kuwasikiliza na kuwasaidia,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles