30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

Hapi aagiza polisi, Takukuru kukamata viongozi

FRANCIS GODWIN,IRINGA

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameagiza jeshi la polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkaoni hapa  kuwakamata viongozi wa mfereji wa umwagiliaji wa  Mlenge ambao wanatuhumiwa kutafuna Sh milioni 75  za mradi huo .

Hapi alitoa agizo hilo juzi, baada ya wananchi kulalamika katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika Kijiji Cha Magombwe.

Wananchi hao, walisema kila mwananchi anayelima katika mradi huo, amekuwa akichangia Sh 10,000, lakini tangu wachangie na kufikisha Sh milioni 75 viongozi hao wametafuna fedha hizo.

Kutokana na hali hiyo, walimuomba mkuu wa mkoa awasaidie kupata fedha hizo walizochangia kwa ajili ya mradi huo .

Akionekana kukasirishwa na kitendo hicho, Hapi, aliagiza jeshi la polisi na Takukuru kuwasaka wahusika wote zaidi ya 10 wanaodaiwa kula fedha hizo na kuwachukulia hatua.

Katika hatua nyinginem Hapi ametoa siku tatu Halmashauri ya Wilaya ya Iringa  kukamilisha ujenzi wa Hospitali wilaya inayojengwa eneo la Igodikafu.

Alitoa agizo hilo baada ya kutembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo kimsingi ilipaswa kukamilika mwezi uliopita kwa maagizo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleman Jafo aliyoyatoa wakati wa ziara yake .

Pamoja na kuagiza ujenzi huo kukamilika hadi Desemba 3 mwaka huu pia,pia aliagiza jeshi la polisi kuwakamata makandarasi watatu ambao wamelipwa fedha na hawaonekani eneo la kazi.

“Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa nakuagiza hawa wakandarasi watatu ambao hawapo site na pesa wamelipwa watafutwe na kuleta kuendelea na kazi wakitokea mahabusu na watafanya kazi usiku na mchana kwa usimamizi wa polisi kuanzia leo,” alisema Mhe Hapi

Alisema Serikali imetoa Sh bilioni 1.5 kutaka wananchi kupata huduma za afya,uongozi wa mkoa hautakubali kuona mtu anacheza na fedha hizo za serikali.

Pia aliagiza kupelekwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kusimamia ujenzi huo huku akimtaka mganga mkuu wa Wilaya na wote wanaohusika na usimamizi wa Hospitali hiyo kushinda eneo la ujenzi huo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles