26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Hamilton ashinda British Grand Prix

Lewis Hamilton

London, England

BINGWA wa mbio za magari kutoka nchini England, Lewis Hamilton, ameshinda ubingwa wa michuano ya British Grand Prix baada ya kumshinda mpinzani wake, Nico Rosberg, huku wote wakitumia gari aina ya Mercedes.

Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Hamilton katika mashindano ya nyumbani nchini England. Katika ushindi huo, Hamilton alitumia saa 1: 34 na sekunde 55, wakati mpinzani wake Rosberg akitumia saa 1:35 na sekunde 12.

Hata hivyo, Hamilton amedai kwamba hakuwa na uhakika wa kushinda kutokana na upinzani aliokutana nao katika michuano hiyo, ila amempa pongezi mpinzani wake kwa changamoto alizompa.

“Sidhani kama kuna mtu anaweza kuwa na furaha kama nilionayo, ukweli ni kwamba nina furaha ya hali ya juu, hii inamaanisha kwamba  British Grand Prix ni michuano bora kwetu.

“Nilikuwa na upinzani mkubwa nikawa na wasiwasi, lakini nashukuru ninazidi kutetea ubingwa wa michuano hii, nilikuwa ninauelewa uwezo wa Rosberg, hivyo nilikuwa na wakati mgumu wa kushinda kutokana na hali ya hewa.

“Mvua iliyokuwa inaendelea ilianza kunipa shida, ila niliweza kupambana hadi hatua ya mwisho,” alisema Hamilton.

Inadaiwa kuwa Hamilton ni miongoni mwa madereva 22 duniani wenye mvuto na idadi kubwa ya mashabiki, baada ya kushinda taji hilo mashabiki walijitokeza kwa wingi wakishangilia kwa kumwinua juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles