26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

HAMAS, ISRAEL WASITISHA MAPIGANO

GAZA, PALESTINA         |       


KUNDI la Hamas limetangaza kusitisha mapigano na Israel katika Ukanda wa Gaza, baada ya siku kadhaa za machafuko ambayo yalisababisha vifo vya mwanajeshi mmoja wa Israel na Wapalestina wanne.

Msemaji wa Hamas, Fawzi Barhoum, amethibitisha uamuzi wa kundi hilo kupitia mtandao wa Twitter kuwa makubaliano na Israel yamefikiwa kwa msaada wa Serikali ya Misri na Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel, Jonathan Conriczs, amesema hangeweza kuyajadili masuala ya kisiasa, lakini amethibitisha kuwa, Israel kwa sasa haifanyi mashambulizi yoyote katika ukanda wa Gaza.

Conriczs amesema jeshi la nchi hiyo tangu juzi lilishambulia maeneo 60, yakiwamo makao makuu matatu ya wapiganaji wa Hamas. Awali Jeshi la Israel lilisema kuwa, mashambulizi yake ya angani yalilenga kujibu shambulizi la ufyatuaji risasi dhidi ya wanajeshi wake waliotumwa kusini mwa mpaka wa Gaza, ambako waandamanaji wa Kipalestina walikusanyika kwenye uzio.

Wizara ya Afya ya Palestina imekiri kupokea miili ya Wapalestina wanne waliouawa na wanajeshi wa Israel kufuatia mapambano hayo.

Kundi la Hamas, ambalo linadhibiti Ukanda wa Gaza, limesema watu watatu kati ya waliouawa walikuwa wanachama wao.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov, aliziomba pande zinazohusika kujizuia na kuwa watulivu.

Vyombo vya habari vya Israel viliripoti kuwa, Misri ilitoa onyo la mwisho kwa Hamas kutoka kwa Israel, likisema kuwa, kama mashambulizi hayatasimama ifikapo wikiendi hii, itafanya mashambulizi mapya ya kijeshi katika ukanda wa pwani.

Hamas na Israel walipigana vita vilivyodumu siku 50 katika mwaka wa 2014. Kwa jumla, Wapalestina 2,250 waliuawa au wakafariki baadaye kutokana na majeraha, wakati Waisrael 74 waliuawa katika mgogoro huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,621FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles