23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yazindua kampeni ya Data Datani

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Simu ya Halotel Tanzania, imezindua Kampeni inayofahamika kwa jina la “Data datani” huku ikiendelea kuwapa kipaumbele watanzania wote mjini na vijini kupitia huduma hii.

Promosheni hii imejikita katika kumpa mteja bonasi ya mb za intanet katika matumizi yake ya kawaida ya Halotel na mteja anaweza kupata hadi GB 5 ambapo waweza kupata huduma hii ukijiunga kifurushi cha intaneti au combo cha siku, wiki na mwezi.

Akizungumza leo Agosti 23, 2024 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio, amesema kuwa Halotel inatambua kuwa mafanikio ya Halotel hayawezi kutenganishwa na wateja wao ambao promoshemi hii ni moja ya huduma ya kumjali mteja wetu na kumpa thamani.

“Tunawahimiza wateja wetu kushiriki kikamilifu katika kampeni hii ambapo kwa kujiunga vifurushi vya intaneti vya combo kupitia *148*66#au kupitia halopesa *150*66#.” amesema Kadio

Kwa upande wa Mkurugenzi wa biashara wa Halotel, Abdallah Salum, amesema kuwa ni vema sasa wateja wetu na watanzania wote waishio mjini na vijijini kuweza kuchangamkia mtandao wetu kwakuwa huwa unawapa kipaumbele kwa kuwapa bonasi mbalimbali kama vile huduma za intaneti na kurahisisha Mawasiliano.

“Halotel inawaletea huduma hii mpya ambapo kila mteja wa Halotel ataweza kupata mb kwa kununua moja ya virushi vyetu na itaweza kumsaidia mteja kufikia malengo katika nyaja ya Mawasiliano na huduma za kifedha,” alisema Salum.

Hata hivyo Halotel imemtambulisha rasmi balozi wake, Elias Barnaba maarufu kama Barnaba Classic ambaye ni mwanamziki na muigizaji hapa nchini ambaye amechaguliwa kuwa mwakilishi wa kampuni katika huduma mbalimbali zinazotolewa watanzania. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles