25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yawageukia wanachuo kwa kuwawezesha kupata bando bure

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel katika juhudi zake za kusaidia Sekata ya Elimu nchini imekuja na ubunifu wa kuwapatia wanafunzi salio lenye thamani ya Sh 1,500 kila mwezi.

Akizungumza Dar es Salaam mapema leo Desemba 6, 2022 Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Abdallah Salum, amesema elimu ni sekta mhimu kwani huibua na kuendeleza vpaji vya wengi, hivyo kwao ni heshima kuwa sehemu ya maendeleo katika eneo hilo.

Kwa kuchangia sekta hii kupitia mradi wa maendeleo ya kijamii, tunaamini kuwa tutapunguza hali ya kutokuwapo kwa usawa na hivyo kufanya maendeleo jumhishi ya rasilimali watu kupata fursa wezeshi zenye tija kidijitali katika masomo na maisha kwa ujumla,” amesema Salum.

Ameongeza kuwa huduma hiyo ni endelevu kwakuwa kampuni inalenga kukuza na kuendeleza wanafunzi wa elimu ya juu kwa kuwapa muda wa maongezi wenye thamani ya Sh 1,500 kila mwezi kuanzia watakapo anza masomo na kumaliza, ambapo takwimu za mwaka 2022 kutoka Tume ya Vyuo Vikuu kwa makadirio kwa sasa kuna zaidi ya wanafunzi 900,000 katika taasisi za elimu za juu.

Aidha, amesema jumla ya vyuo vikuu 280 vimejumhishwa katika mpango huo wa Halotel.

Pamoja na hayo yote kampuni imeandaa tamasha litakalohusisha burudani mbalimbali na kutoka kwa wasanii.

Kwa upande wa Afisa Masoko wa Halopesa, Roxana Kadio, amesema kuwa wanahakikisha wanafunzi wa chuo wanapata huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia Halopesa bila tozo za Serikali.

“Kampeni hii itaendeshwa kwa muda wa miezi sita kuanzia mwezi huu wa Desemba, ambapo wanafunzi wa vyuo wanaotumia Halopesa, wataweza kufanya miamala yenye thamani isiyozidi Sh 30,000,” amesema Kadio.

Kwa upande wa Rais wa Wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Spencer Minja, ameipongeza Kampuni ya Halotel kwa kuja na ubunifu huo, ambao utasaidia wanafunzi kusoma kidijitali kwa kujiunga na vifurushi vya intenenti.

“Kupata salio la Sh 1,500 kila mwezi itasaidia kwa wanafunzi wengi ambao kipato chao ni kidogo,” amesema Minja.

Aidha, hivi karibuni kampuni ya Speedtest Global Index ilitoa ripoti yake na kuonyesha kuwa Halotel imeongoza kwa kuwa na mtandao wenye kasi zaidi ukilinganisha na mitandao mingine katika kipindi cha robo tatu zote za mwaka zilizoishia Septemba, mwaka huu mwezi Septemba iliongoza kwa kuwa na intaneti yenye kasi ya 17.63 Mbps, ikifuatiwa na Vodacom (13.63mbps) na Airtel 11.61Mbps.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles