26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 26, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Halotel yatoa tiketi kwa washindi safari ya Dubai

Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Halotel imewakabidhi tiketi za ndege washindi wa ‘Vuna Pointi Twenzetu Dubai’ kwa ajili ya safari ya kwenda Dubai katika kusheherekea msimu wa wapendanao (Valentine)

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari13, 2025 makao makuu ya kampuni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio amesema wanajivunia kutangaza kumalizika kwa kampeni hiyo ya kipekee.

“Kampeni yetu ya Vuna Pointi Twenzetu Dubai, ilikua inamuwezesha mteja kuvuna pointi kupitia namba ya bahati na kumuwezesha mtumiaji wa Halotel kupata nafasi ya kujishindia nafasi ya kwenda Dubai na mwenza wake au mtu yeyote atakayemchagua,”amesema Kadio.

Ameongeza kuwa katika kutamatisha kampeni hiyo, wamepatikana wateja wawili walioshinda na wamepata bahati ya kwenda Dubai kwa siku tatu msimu huu wa wapendanao.

Amesema kampeni hiyo ni sehemu ya dhamira kwa kampuni kuimarisha uzoefu wa wateja na kuwalipa wateja wao waaminifu wananachofanya kupitia shindano hilo ni kuwapa nafasi ya kuishi na kupata uzoefu wa Dubai, mji maarufu kwa anasa, tamaduni na uvumbuzi.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Kitengo cha huduma kwa wateja Halotel, Sharon Kessy amesema kampuni inaendelea kuimarisha sifa yake kama chapa inayojali wateja kwa kutoa sio tu huduma bora za mawasiliano bali pia uzoefu unaoboresha maisha ya watumiaji wake hivyo
jamii ijiandae kushiriki mashindano mengine ya kuvutia mwaka huu.

Naye mshindi wa tiketi hiyo, Raphael Myombo amesema ndoto yake imetimia kwani hakuwahi fikiria kama angeweza kufika Dubai lakini kupitia Halotel amefanikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
596,000SubscribersSubscribe

Latest Articles