Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania katika kusherehekea miaka 7 ya huduma, imeendelea kuwahakikishia wateja wake ubora na kasi ya mtandao wake kwa kuwapa huduma zenye ubunifu na kubuni bidhaa mpya zenye lengo la kuwazawadia watanzania wanaotumia mtandao huo mjini na vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2022, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano Halotel, Sakina Makabu, amesema kuwa wamezindua kampeni mpya inayojulikana kama “7 bang bang” kwa wateja wao ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kwa kutumia huduma zao hadi hivi sasa inapotimiza miaka 7 ya utoaji huduma.
“Kampeni hii itawawezesha wateja kushiriki katika Promosheni itakayowawezesha wale ambao watajiunga na mtandao wetu kushiriki bahati nasibu na kushinda zawadi mbalimbali kama vocha, yenye thamani mpaka Sh 100,000,” amesema Sakina.
Amesema zawadi ambazo wataweza kujishindia kwa kutumia mtandao wa Halotel pamoja na kuongeza salio ni pamoja na simu janja aina ya Samsung Galaxy A53 na A73, Televishen janja nchi 50, jokofu, Wifi Router ya 4G ambalo draw ya mwisho itakayochezeshwa ndani ya wiki 10 ni gari mpya aina ya IST.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo Cha huduma kwa wateja wa Halotel, Patrick Rwegoshora, amesema kuwa Promosheni hii ni maalum kwa wateja wetu wote ikiwa ni moja ya ishara ya kuwashukuru kwa kuchagua na kutumia mtandao wa Halotel.
“Katika promosheni hii, mteja wetu anachotakiwa kufanya ni kuweka voucha zaidi katika lakini ya Halotel na moja kwa moja atakuwa katika nafasi ya kuingia kwenye droo ya bahati nasibu na kuweza kujiweka katika njia nzuri ya kuwa mshindi,” amesema Rwegoshora.
Aidha, Halotel itatoa washindi 95 kila wiki, washindi 32 kila mwezi, washindi 16 wa robo hii ya mwisho wa mwaka na mshindi mmoja wa mwisho wa promosheni ataweza kujishindia gari mpya aina ya IST , hivyo washindi 143 watapata zawadi mwisho wa Promosheni hiyo.
Wakati huo huo Mteja wa Halotel anaweza kutumia huduma za HaloPesa katika kuingia kwenye droo ya ushindi kwa kununua vocha kupitia HaloPesa.
Afisa Masoko wa HaloPesa, Roxana Kadio amesema kuwa, mwisho wa wiki ya Oktoba 14, hadi Oktoba 16, mwaka huu.
“Wateja wa HaloPesa wataweza kutumia huduma hii bila tozo na Mteja kuweza kutumia Miamala kupitia HaloPesa App na kurudishiwa gharama za tozo alizokatwa huku Halotel ikitoa huduma ya kizazi Cha nne Cha huduma za mtandao wa 4G katika maeneo mengi nchini,” amesema.