Halotel yaja kidigitali, yazindua App ya HaloPesa

0
1053

Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

Kampuni ya Halotel Tanzania kupitia huduma yake ya HaloPesa imeendelea kujikita kidigitali zaidi kwa kuzindua huduma ya HaloPesa App na kampeni ya #ChillaxNa HaloPesa App.

Kutokana na hali hiyo wateja wote wa Halotel wanaweza kupakua Halopesa App kupitia simu zao za mkononi.

Akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha biashara cha HaloPesa, Magesa Wandwi amesema HaloPesa App inampa uhuru mteja kutumia simu janja yoyote kwa kuweka namba yake ya simu na neno la siri na kufanya miamala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuma pesa kiurahisi na usalama kwa namba ambazo wamezihifadhi kwenye simu zao za mkononi.

“HaloPesa App imetengenezwa Kwa ubunifu na kuzingatia sana urahisi katika utumiaji ili kuwapa wateja wetu uzoefu wa tofauti wanapotumia huduma zetu kupitia HaloPesa App ya ChillaxNa HaloPesa App.

“Wateja sasa wanaweza pia kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kihurahisi kwa kuskani QR code  kama  MasterPass bila kusahau kurudisha miamala ya kifedha endapo mteja atakosea kutuma au kufanya malipo kwa urahisi, haraka na salama zaidi bila kutumia data,” amesema Magesa.

Amesema kuwa wateja wote wa Halotel wakipakua HaloPesa App watajipatia bando la GB moja na dakika 10 za maongezi bure ambapo wataweza kutumia wapendavyo ndani ya siku saba.

Ameongeza kuwa mtandao wa mawakala wa mtandao huo umeendelea kukua kwa kasi na kwamba hadi sasa ina zaidi ya mawakala 52,000 nchi nzima na hivyo wateja wao wanaweza kupata huduma kwa urahisi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here