32.2 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

Halotel Tanzania yakabidhi gari jipya la promosheni ya 7bang bang

*Ni mshindi wa Grand draw wa promosheni ya 7 bang bang

*Zawadi mbalimbali zimetolewa kwa jumla ya washindi 143 wa promosheni ya “7 bang bang”

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano nchini ya Halotel Tanzania PLC leo imekabidhi zawadi kwa mshindi mkuu aliyejishindia gari aina ya IST Mpya wa draw kubwa ya mwisho ya promosheni ya wateja iliyokuwa na jina la 7bang bang.

Promosheni hiyo ya “7 bang bang” iliendeshwa kwa wiki 10 na kuwapa fursa wateja wote wa Halotel ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kwa kutumia huduma zao kwa miaka saba ya utoaji huduma bora za Mawasiliano hapa nchini.

Tangu kuanza kwa promosheni hiyo ya bahati nasibu zaidi ya washindi 140 wameweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Vocha yenye thamani mpaka laki moja, Simu janja aina ya Samsung Galaxy A53 na A73, Televisheni janja zenye inchi 50.

Akizungumza wakati wa hafla makabidhiano ya gari jipya aina ya IST Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel Abdallah Salum, alisema, “Leo hii, tuna mshindi aliyebahatika kujishindia gari jipya kabisa kwa kushiriki katika shindano letu la promosheni ya 7 bang bang.

Tumeona itakuwa vizuri ikiwa zawadi hii ya gari ikakabidhiwa wakati tukiwa tunamalizia msimu wa sikukuu” ukiwa sambamba na kuwashukuru wateja wetu wote kutumia huduma za Mawasiliano kutoka Halotel sambamba na kuadhimisha miaka 7 kutoa huduma hapa nchini.

Katika tukio hili la makabidhiano, zawadi kubwa kuliko zote ya gari jipya aina ya IST ilikabidhiwa kwa mshindi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi rasmi gari hilo alisema, Mkurugenzi wa Biashara Halotel, Abdallah Salum alisema siku ya leo tunayo furaha sana kuweza kumkabidhi mteja wetu ambaye ni mshindi mkuu wa gari mpya aina ya IST katika droo kubwa ya mwisho ya promosheni iliyokuwa na jina la 7 bang bang.

“Sholastika Sostenes Haule, napenda kukupa pongezi kubwa sana na unavyochukua gari lako, ninakuasa kutumia zawadi hii ambayo ni fursa adimu, katika kupiga hatua kimaisha na isiwe mwisho wa jitihada zako. Hii iwe hatua kwako, kukufanya  uendelee kuweka bidii ili uendelee kupanda zaidi kimaisha,” amesema

Aidha’ Salum, alitumia fursa hiyo kuwahimiza wateja wao waendelee kutumia mtandao wa Mawasiliano wa Halotel ambao unaendelea kuwa na ubinifu kuhakikisha kila mteja anafurahia huduma za mawasiliano kwa ubora wa hali juu kutoka Halotel.

Kwa upande wake, Sholastika Sostenes Haule aliishukuru kampuni ya Halotel, na kuwasihi wateja kuendelea kutumia mtandao wa Halotel na kushiriki katika promosheni zinazotolewa kampuni ya Halotel ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali zinazokuwa zinatolewa kupitia promosheni hizo.

Sambamba na tukio hilo la kukabidhi zawadi ya gari kwa mshindi, Kampuni hiyo ilitumia fursa hiyo kufanya uzinduzi wa duka jipya na la kisasa linalopatikana Palm Village Mall iliyopo kando ya barabara ya Mwai Kibaki Mikocheni, Dar es Salaam ambapo wateja wa Halotel sasa watapata huduma zote za Halotel katika Duka hilo.

Duka hili lililoboreshwa kwa njia ya kidigitali litatoa huduma zote zitakazojumuisha huduma ya kusajili laini mpya na kusalijili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole, ubadilishaji wa laini kutoka 3G kwenda 4G, Huduma za vocha (elektroniki na kukwangua) uthibitishaji wa namba za simu, huduma za HaloPesa, bidhaa za Halotel kama router na huduma zote za ziada na za baada ya mauzo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara, Abdallah Salum  amesema “Uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa Halotel wa kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na kutimiza ahadi yake ya kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa na huduma kwa ukaribu na urahisi zaidi.

“Tunapenda kuwakaribisha wateja na watanzania wote kwa ujumla katika duka letu la Halotel hapa Palm Village Mall kuweza kupata na kufurahia huduma bora za Halotel katika duka hili,” aliongeza Abdallah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles