26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Halotel kujivunia miaka mitano ya mafanikio kufikisha idadi ya watumiaji zaidi ya milioni sita.

Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

Kampuni ya Viettel kwa jina la biashara Halotel, siku ya leo inasheherekea maadhimisho ya miaka mitano ya utoaji huduma za mawasiliano Tanzania, Kwa muda wote wa utoaji huduma imeweza kufikia malengo kwa viwango vya juu ikiwemo kuongeza watumiaji wa mtandao huo.

Kutokana na ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya robo ya pili ya mwaka, Halotel imefanikiwa kufikisha idadi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano zaidi ya milioni sita mpaka mwezi juni mwaka 2020.

Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mkubwa wa serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji, pia watanzania kwa ujumla ambao ni wateja wetu, wafanyakazi wa Halotel pamoja na ubunifu mkubwa wa kampuni kwa ujumla kwa kutengeneza huduma zinazokidhi na mahitaji ya watuamiaji.

Akiongea na waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo alisema, “Halotel imekuwa ikitoa huduma ya intaneti kwa shule za msingi na sekondari za serikali, imeweza kuunganisha mawasiliano kwa ofisi za serikali kuanzia ofisi za wilaya, vituo vya polisi na ofisi za posta kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufasaha,” alisema Trung

Halotel ni mtandao wa kwanza kupeleka mawasiliano kwa vijiji 4,000 ambavyo havikuwa na mawasiliano toka Tanzania kupata uhuru ambapo matokeo yake imesisimua maendeleo ya wakazi wa vijiji hivyo.alisema naibu Mkurugenzi huyo.

Kama wawekezaji wengine Halotel imekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia jamii kufikia maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya kiafya, elimu, mawasiliano, michezo, kilimo na watu wenye uhitaji maalumu kwenye jamii zetu.

‘Pia tunafurahia kuona watanzania hivi sasa wameshika nafasi kubwa za uongozi (menejiment) makao makuu na katika matawi yetu ya nchi nzima. Haya ni mafanikio makubwa kuona Halotel inaendeshwa na kusimamiwa na watanzania na sasa ni wasaa wao wa kuonesha uwezo na maarifa yao kuleta huduma bora zaidi,” alisema Trung

Katika kusheherekea miaka mitano, Halotel imezindua ofa maalum zitakazowawezesha watanzania kuwasaliana kwa punguzo kubwa. Hii ni mara ya kwanza kwa Halotel kutoa ofa kubwa kwa wateja wake na ofa hizo zinajulikana kama, “DABO BANDO” na KUONGEA BURE HALOTEL KWENDA HALOTEL pia kwa wateja wetu watakua wakipata zawadi mbalimbali ikiwemo vocha watakapo tembelea maduka ya halotel yaliyoko nchi nzima ndani ya mwezi huu.

“Tunapenda kuwapongeza wateja wetu kwa kuchagua mtandao wa Halotel kwa miaka yote mitano ya utoaji wa huduma za mawasiliano na hivyo tunapenda kutoa ofa hii kama zawadi kwa wateja wetu.

“Ambapo ofa maalumu ya DABO BANDO, mteja wa Halotel atapata mara mbili ya kifurushi cha siku cha muda wa maongezi au intaneti kuanzia tarehe 15 Oktoba mpaka Oktoba 31, 2020. Kifurushi cha siku kinaweza kuunganishwa kwa kupiga menyu ya Halotel 14866# kupitia muda wa maongezi au Halopesa. Kwamfano mteja wa Halotel akijiunga na kifurushi cha siku cha intaneti cha GB 1 atapata GB 1 nyingine bure,” alisema Trung

Mbali na Ofa za Halotel, Trung alizindua ofa maalum ya Halopesa ya “kurudishiwa asilimia 50 ya makato ya kutuma pesa”, kwa mtandao wa Halotel na mitandao mingine kwa muda wa siku tatu kuanzia terehe 15 hadi 17 Oktoba 2020. Pia wakala na washirika wa Halopesa wataweza kupata zawadi na hati za shukrani.

Pia alisema kuwa mbali na kutoa huduma bora kwa gharama nafuu. Halotel wataendelea kuleta huduma zenye tija ambazo zitakidhi mahitaji ya wateja na hicho ndicho kipaumbele cha kampuni yao.

Halotel ni tawi la kampuni ya kivietnam Viettel Group ambayo imeanza kutoa huduma za mawasiliano nchini tangu Oktoba 15, 2015 ambayo imeweka mkazo kuunganisha vijiji ambavyo havikuwa na mawasilia ambapo asilimia 80 ya watanzania wa
naishi huko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles