Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital
Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kupitia huduma yake ya kifedha ya Halopesa, katika kuelekea kipindi cha Sikukuu imeamua kusherehekea msimu huu kwa kutembelea kituo cha kulelea watoto maalum cha Salt Special Centre kilichopo Mbezi Msakuzi.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Desemba 20, katika kituo hicho, Afisa masoko wa Halotel, Roxana Kadio, amesema kuwa ninfursha kubwa kusherehekea na ndg zetu hawa ambao wanalea watoto wenye uhitaji maalumkatika kipindi hiki mhimu cha Sikukuu.
“Katika kipindi hiki cha Sikukuu tumeona ni vema kuwa karibu na kituo hiki chenye takribani watoto 42 wanaosumbuliwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwa ni pamoja na kupata pamoja chakula cha mchana kwani ni jukumu letu kurudisha shukrani kwa jamii,” amesema Roxan.
Aidha, Halopesa pamoja na kuwatembelea Salt Special Centre, imewazawadia vitu mbalimbali kama nguo, chakula, sabuni, kulingana na mahitaji ya kituo husika huju Halopesa ikiamua kujumuika nao pamoja chakula cha mchana ambapo Halopesa imefanya hivyo kwa kuonyesha upendo, thamani na kujali katika jamii kwa ujumla.
Ameongeza kuwa Halopesa inafurahia kujumuika na marafiki na itaendelea kuangalia namna nyingine zaidi ya kuonyesha ulimwengu thamani na upendo ikiwa pamoja na kuboresha huduma za kifedha kupitia simu ili ziwe bora kwa ajiri ya wateja wa halotel.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa kituo hicho cha Salt Special Centre, Rebecca Lebi, amesema kuwa ni furaha kubwa mno kupata watu wanaotambua thamani, utu na na kujali utu wa watu wengine kama walivyo fanya Halotel.
“Nina furaha mno kuona kampuni kama Halotel kutambua thamani yetu kisha kuamua kuja kututembelea na kutuletea zawadi mbalimbali katika kipindi hiki cha sikuu, hii itasaidia na sisi kujiona ni sehemu ya jamii kama jamii zingine hivyo tunaomba taaisi nyingine zijitokeze kwa kuchangia mahaitjai mbalimbali katika kituo chetu,” amesema.