26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

HaloPesa, Umoja Switch kutoa huduma ya fedha kwa ATM

Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

Kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia na uchumi, Halopesa imeendelea kutanua wigo wa kutoa huduma zake za kifedha nchini ikizingatia pia mkakati wa kitaifa wa ujumuishwaji wa wananchi katika matumizi ya mifumo rasmi ya kifedha chini.

Ikiwa ni mwendelezo wa kuwafikia na kuwapa wateja wa Halopesa huduma bora kwa urahisi na uhakika, Halotel kupitia huduma yake ya HaloPesa imeingia ubia na Kampuni ya UmojaSwitch kutoa huduma kwa wateja wa HaloPesa ya kutoa fedha kupitia ATM za Umoja zilizoko kote nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Makao Makuu ya Halotel, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Magesa Wandwi, amesema kuwa ni hamasa na lengo letu kuhakikisha kuwa wataendelea kutumia miundombinu ya teknolojia na fursa zote zilizopo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta hiyo ya huduma za kifedha.

“Tuwapa wateja wetu huduma bora na za uhakika na nifuraha yetu leo kushirikiana na UmojaSwitch kuzindua rasmi huduma hii ambayo itawawezesha wateja wa HaloPesa kutoa fedha kwa urahisi na uhakika zaidi kupitia ATM za Umoja zaidi ya 250 zilizopo maeneo mbalimbali kote nchini.

“Tunapenda kuwasisitizia wateja wetu kuwa Huduma hii haitakuwa na makato ya ziada tofauti na makato ya kawaida ya kutoa pesa kwa wakala wa kawaida, lakini pia huduma hii haitahusisha matumizi ya internet pale ambapo mteja atakuwa anatoa fedha kwenye ATM za Umoja,” amesema Magesa.

Amesema kuwa huduma hiyo pia itatumiwa na mawakala zaidi ya 50,000 waliosambaa nchini kote.

” Kwa pamoja tutaendelea kuwahudumia wateja wetu wa Halopesa zaidi ya milioni Mbili waliopo mijini na vijijini.

“Mteja wa Halopesa atapitia hatua za kawaida kutoa pesa kwa kupiga 15088# kisha kuchagua ‘2’, (Kutoa Pesa ), Kisha chagua tena “2” (UmojaATM), ataendelea na kuweka kiasi na namba yake ya siri ya Halopesa, baada ya hapo atapata ujumbe wenye namba ya siri ya uthibitisho ambayo ataitumia kutoa fedha katika ATM za Umoja, “Ameongeza Magesa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa UmojaSwitch, Danford Mbilinyi, amesema ushirikiano na Halopesa utaongeza upatikani wa huduma za kifedha kirahisi nchini kupitia ATM zetu zaidi ya 250 zilizoenea nchi nzima na kwamba wateja wa HaloPesa wana fursa nyingine ya uhakika sasa ya kupata fedha muda wowote mahali popote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles