33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri ya Mwanga yapitisha bajeti ya Sh bilioni 30.3

Na Safina Sarwatt, Mwanga

Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, wamepitisha mapendekezo ya rasimu na mpango wa bajeti ya Sh bilioni 30.3 ya Mwaka wa fedha 2021/2022.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Salehe Mkwizu, akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Februari 22, mwaka huu katika ukumbi wa kituo cha walimu Mwanga.

Mkwizu amesema kuwa kiasi cha fedha hizo Sh bilioni 5.066 ni mapato ya ndani, Sh bilioni 19.855 ni Mishahara, Miradi ya Maendeleo Sh bilioni 4.104 na Ruzuku ya matumizi ya kawaida Sh bilioni 1.315.

Wakichangia bajeti hiyo baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo, Amiri Sarumbo, Diwani wa Kata ya Kirongwe na Kiende-Mvungi Diwani wa Kata ya Kwakoa walisisitiza kuongezwa makusanyo ya ndani kutoka Sh bilioni 5 hadi kufikia Sh bilioni 10 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo eneo la Bwawa la Nyumba ya Mungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles