27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri nchini zatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya WAVIU

Na Mwandishi Wetu, Tanga

Naibu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga amepongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 3.5 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 3.2 kwa mwaka 2021.

Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga akiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya alipotembelea shule ya Msingi Majani Mapana na shule ya Sekondari Nguvu Mali kujionea utekelezaji wa mradi wa TIMIZA MALENGO

Hayo yamesemwa Mei 28, 2022 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa wa Tanga ya Mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye bajeti mpya ya Serikali 2022-2023 itakayoanza Julai mwaka huu wa saba ameongeza fedha eneo kutoka Sh billion 1 mpaka Sh billion 1.8,” amesema Nderiananga.

Aidha, Naibu Waziri Nderiananga ameshauri Halmashauri za wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha za Mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI nakwamba hatua hiyo itasaidia  kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo vizuri.

Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza, Bahati Mohamed ambaye ni Katibu wa Konga Jiji la Tanga alipotembelea katika ziara yake kujionea shughuli za kiuchumi za WAVIU.

“Wananchi msiogome kujitokeza kupima virusi vya UKIMWI, mpime mjitambue afya zenu. Kama Kauli mbiu inavyosema Pima VVU, Jitambue,Ishi.

“Mabinti mnao toa elimu rika, endeeleni kuwaelimisha mabinti wenzetu. Asilimia kubwa ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI yapo kwa vijana na asilimia 80% ya hao vijana ni mabinti lazima tuendele kuelimishana,”amesema Nderiananga.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kaspar Mmuya amesema Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI ambao wamejitokeza na kujitangaza na kusema wako tayari kushirikiana na serikali kutoa elimu (NACOPHA) ni baraza muhimu.

“Hili Baraza ni rasilimali kubwa sana kufikia malengo yetu, wanaishi kwa mfano na wanamalengo na wanatusaidia hata wale walioacha dawa kwa sababu mbalimbali wanawatafuta na kuongea nao na kuwarudisha kwenye dawa.

“Ninaomba hizi afua mbalimbali za UKIMWI zinazofanyika, maelekezo yatoke mradi wowote unahusu mambo ya UKIMWI washirikiane na NACOPHA. Hawa wanauwezo wa kufikia walengwa mpaka ndani kijijini na wanatusaidia kufikia malengo ya taifa kwa kutumia muda na vizuri,” amesema Mmuya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles