Halmashauri Hai yapata Makamu Mwenyekiti mpya

0
1755
Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai (kushoto), akimkabidhi mavazi maalumu Makamu Mwenyekiti mpya, Elingaya Massawe. PICHA na Upendo Mosha

Upendo Mosha, Hai

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, limefanya uchaguzi na kumchagua, Elingaya Massawe kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Baraza hilo limefanya uchaguzi huo leo Ijumaa Agosti 30, chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wake Helga Mchomvu.

Massawe aliibuka mshindi baada ya kupata kura 15 kati ya 22 zilizopigwa na kumshinda mshindani wake Deo Kimaro ambaye alipata kura saba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here