27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

HALMASHAURI BUNDA YATUMIA BILIONI 30/- MWAKA 2016/17

Na Ahmed Makongo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Bunda ilikadiria  kutumia  zaidi ya Sh bilioni 39.3. kutoka serikali kuu na kwenye vyanzo vyake vya ndani katika mwaka wa fedha 2016/17.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Amos Kusaja,   alisema hadi Juni 30 mwaka huu, makisio yote yalikuwa ni kutumia zaidi ya Sh bilioni 41.5 na kuanzia Julai 2016 hadi Juni mwaka huu zimetumika  zaidi ya Sh bilioni 28.9 sawa na asilimia 69.76 ya makisio ya matumizi yote.

Alikuwa akizungumza kwenye  kikao cha mwaka cha baraza la madiwani mjini Bunda.

Alisema bakaa iliyokuwapo wakati wa kufunga mwaka wa fedha wa 2015/2016 ilikuwa Sh  bilioni 2.1 na kufanya   mapato yote kwa ajili ya matumizi mengineyo   na miradi ya maendeleo kuwa zaidi ya Sh  bilioni 41.5.

“Bakaa iliyokuwapo wakati wa kufunga mwaka wa fedha wa 2015/2016 ni Sh 2,150,105,777 na kufanya   mapato kwa ajili ya matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo kuwa Sh  41,532,391,729,” alisema.

Alisema mapato ya vyanzo vya ndani makisio yalikuwa ni zaidi ya Sh  milioni 850.8 na hadi kufikia   Julai mwaka huu, zilikuwa zimekusanywa zaidi ya Sh milioni 737.1.

Alisema kuwa ruzuku ya mishahara makisio yalikuwa ni zaidi ya Sh bilioni 30.7 na hadi kufikia   Julai mwaka huu, walikuwa wamekusanya zaidi ya Sh bilioni 21.5.

Kusaja alisema  ruzuku ya matumizi mengineyo makisio yalikuwa ni zaidi ya Sh bilioni 1.3 na hadi kufikia   Julai zilikuwa zimekusanywa zaidi ya Sh bilioni 1.2.

Kuhusu ruzuku ya miradi ya maendeleo alisema  makisio yalikuwa ni zaidi ya Sh bilioni 6.4, ambapo kufikia   Julai mwaka huu, zilikuwa zimekusanywa zaidi ya Sh bilioni 5.3.

Alisema  makisio yote yalikuwa ni zaidi ya Sh bilioni 39.3 na   hadi kufikia   Julai mwaka huu zilikuwa zimekusanywa zaidi ya Sh bilioni 28.8 sawa na asilimia 37.33 ya makisio yote.

Hata hivyo, alisema  kulikuwa na chanagamoto mbalimbali katika kukusanya mapato ya halmashauri kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani,  mojawapo ikiwa ni upungufu wa vifaa vya elektroniki   vya kukusanyia mapato hayo.

Changamoto nyingine ni   kukosekana   tafsiri ya matamko ya serikali yanayotolewa kuhusu ukusanywaji mapato kama vile ushuru wa mazao na ukosefu wa miundombinu kwenye minada.

Alisema halmshauri hiyo itabuni vyanzo vingine vya mapato jambo ambalo madiwani wote wakiongozwa na Mwenyekiti   Isack Mahera walilikubali ili kusaidia kuongeza mapato  kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles