30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Hali maambuzi ya VVU nchi za SADC inatisha

KOKU DAVID – DAR ES SALAAM

Nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), zinachangia kwa asilimia 45 idadi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mratibu wa Programu za Kikanda na Kimataifa, Renatus Kihongo, alisema kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2014 kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS GAP) nchi zilizoko kwenye ukanda wa SADC ndizo kwa sehemu kubwa zimeathirika zaidi na Ukimwi.

Alisema nchi hizo ni sehemu ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika lenye zaidi ya asilimia 65 ya watu walioambukizwa Ukimwi duniani na idadi ya watu wake ni asilimia 12 tu.

“Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi ya mwaka 2014, dunia inakadiriwa kuwa na nchi 196, nchi tisa za SADC zinachangia asilimia 45 ya idadi ya watu wanaoishi na VVU wakati nchi saba zinachangia kwa asilimia 42 ya maambukizo mapya huku nchi nane zikichangia kwa asilimia 41 ya vifo vinavyotokana na Ukimwi,” alisema Kihongo.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wanachama wa SADC ambazo zilisaini Azimio la Maseru ili kushirikiana katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

Kihongoa alisema miongoni mwa sababu za kutiliana saini azimio hilo ni mwingiliano mkubwa uliopo baina ya raia wa nchi wanachama kutokana na shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aliongeza kuwa mwingiliano huo unasababisha kuwepo kwa vihatarishi vingi vya kuambukizwa na kuambukiza VVU hali inayochangia kuongezeka kwa maambukizo mapya kutoka nchi moja hadi nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles