24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

HAKI ZA WANAWAKE NI HAKI ZA BINADAMU

New York, Marekani


KATIBU Mkuu, Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki moon amesema licha ya maboresho katika nafasi za uongozi, hata hivyo pengo la kijinsia katika uchumi ni kubwa kwani idadi ya wanamume ni kubwa kuliko wanawake.

Kimoon ametoa ujumbe huo katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, na kueleza kuwa haki za wanawake ni haki za binadamu.

Ujumbe huo wa kiongozi huyo ulisema nyakati hizi za taabu duniani, machafuko hayatabiriki na huku haki za wanawake na wasichana zinazidi kupungua na kuwekewa vikwazo.

Aidha, kuwawezesha wanawake na wasichana ni njia pekee ya kulinda haki zao na kuhakikisha kuwa wanaweza kutambua uwezo wao.

Katika ujumbe huo alisema kukosekana kwa usawa wa kihistoria katika mahusiano ya madaraka kati ya wanamume na wanawake kunachochewa na kuongezeka kwa utofauti kati ya jamii na nchi zinazoongoza kwa ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana.

Taarifa hiyo ilisema duniani kote, mila, maadili ya kitamaduni na dini vinatumika vibaya kuondoa haki za wanawake. Uwepo wa ubaguzi wa kijinsia na vitendo vya chuki dhidi ya wanawake.

“Haki za kisheria za wanawake ambazo hazijawahi kuwa sawa na wanamume katika mabara yote zinazidi kukandamizwa zaidi.

“Haki za wanawake juu ya miili yao wenyewe inahojiwa na kudharauliwa. Wanawake mara kwa mara wamekuwa walengwa kwa vitisho na kunyanyaswa katika mitandao na kwenye maisha yao halisi” alisema Ki moon na kuongeza.

“Mbaya zaidi, watu wenye msimamo mkali na magaidi hujenga itikadi zao kwa wanawake na wasichana na kuwateka kwa ajili ya vitendo vya ngono, unyanyasaji wa kijinsia na kuwalazimisha ndoa za utotoni na utumwa.

Katibu Mkuu huyo alisema ni lazima kubadili hali hii, kwa kuwawezesha wanawake katika ngazi zote, kuwezesha sauti zao kusikilizwa na kuwapa mamlaka juu ya maisha yao wenyewe na juu ya mustakabali wa dunia yetu.

“Kukataa haki za wanawake na wasichana ni vibaya kwa sababu  ina athari kubwa  kijamii na kiuchumi. Usawa wa kijinsia unaathari ya kuleta mabadiliko ambayo ni muhimu kwa jamii na uchumi.

“Kuwapatia wanawake elimu na afya ni faida kwa familia zao na jamii ambayo itaendelea kwa vizazi vijavyo.”ilisema taarifa hiyo na kuongeza. Mwaka wa ziada katika shule inaweza kuongeza asilimia 25 ya mapato ya msichana siku zijazo.

“Wakati wanawake wanashiriki kikamilifu kwenye sekta ya ajira, inatengeneza fursa na kuchangia ukuaji wa uchumi,”alisema Katibu Mkuu huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles