Haki za Binadamu kusimamia wananchi kudai Katiba Mpya

0
1387

Leonard Mang’oha na Magreth Msangi (Tudarco), Dar es Salaam



Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga, amesema kituo hicho kipo katika mpango wa kuwajengea uelewa wananchi ili wadai Katiba mpya wao wenyewe baada ya mchakato wake kusimama tangu mwaka 2014.

Henga ametoa kauli hiyo leo Jumatano Septemba 26, wakati wakisherehekea miaka 23 tangu kuanzishwa  kwa kituo hicho ambacho amedai kimekuwa kimbilio la wananchi wengi.

Amesema hawataacha kupaza sauti kudai Katiba hiyo kwa sababu imeligharimu taifa fedha nyingi pamoja na kukusanya maoni ya wanachi ambayo hawataki yapotee.

“Hatutaacha kudai Katiba Mpya ila kwa sasa tunachokifanya ni kuelimisha wananchi ili wao wenyewe waweze kuidai katiba hiyo, kama mnavyojua mchakato huu umechukua  fedha nyingi na wananchi tulitoa maoni ambayo hatutapenda yapotee.

“Sisi tulianzisha mchakato wa Katiba mpya nchini uliyosababisha vuguvugu kubwa la watu kushiriki katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba mwaka 2014, hata kabla ya Serikali kuanzisha mchakato huo,” amesema.

Aidha, amesema kumekuwa na hali mbaya ya haki za binadamu katika kipindi cha miaka mitatu ikilinganishwa na wakati walipokuwa wakisherehekea miaka 20 ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here