Shirika la Haki Elimu limesema tukio la adhabu ya kikatili aliyopewa mwanafunzi Sebastian Chinguku ni sehemu tu ya matukio mengi ya ukatili wanayofanyiwa wanafunzi mashuleni.
Mbali na hilo wamesisitiza kuwa matukio hayo ya kikatili yamezifanya shule kutokuwa sehemu rafiki na salama kwa wanafunzi na hivyo kuwa na athari kubwa katika juhudi zao za kujifunza