25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Habib Mchange: mabadiliko sheria za vyama vya siasa dawa ya viongozi ving’ang’anizi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya serikali ya Alliance for Development Organisation (ADO), Habib Mchange, amesema Muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa utakuja na majibu kwa viongozi hasa wale wanaong’ang’ania madarakani na kwa wanachama wengi wa vyama hivyo tofauti na wengine wanaoupinga.

Muswada huo, ni ule wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa uliowasilishwa bungeni Novemba mwaka jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 6, Mchange amesema muswada huo ukipitishwa utatatua malalamiko ya wanachama wengi kwani watakuwa wamepewa nguvu za kumshtaki kiongozi wao yeyote akienda kinyume na katiba ya chama chao kwa msajili wa vyama vya siasa.

“Naunga mkono muswada huu wa mabadiliko kwani kuna vifungu ndani yake ambavyo mimi binafsi naona vinafaa na vitatoa nafasi ya kubadilishana uongozi na vitawalazimisha viongozi wakuu wa vyama kuwa na ukomo wa madaraka.

“Siwashangai waliofungua kesi mahakamani kwani haki yao kikatiba lakini je, unafungua kesi kuhusu nini muswada huu utatoa kibali kwa mkaguzi mkuu wa serikali kuhoji fedha za ruzuku wanazopewa vyama vya siasa  kila mwezi wanazipeleka wapi na kama haijulikani basi wataadhibiwa kutokana na sheria inavyosema,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles