27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

HABBAT SODA HUSAIDIA WAGUMBA, WANAONYONYOKA NYWELE

WIKI iliyopita tulizungumzia maradhi ambayo mafuta ya habbat soda yanaweza kukabiliana nayo, ambapo tuliona magonjwa sita, leo tunaendelea na makala hii. 

  1. Hutibu maambukizi

Maambukizi ya aina yote hupigwa na kinga ya mwili hasa na seli nyeupe za damu ndizo zinazohusika na kazi hiyo. Kwa kuiongezea nguvu kinga ya mwili moja kwa moja, mafuta ya habbat soda yanausaidia mwili wako kupigana na maambukizi kutoka kwenye nywele kichwani mpaka kwenye kucha. Hii ni sifa ya pekee ya habbat soda ambayo imekuwa ikijulikana kuwa nayo katika historia yote ya dunia tangu enzi, hata leo bado ni moja ya dawa za asili zenye nguvu ya kupigana na maambukizi ya aina nyingi ya mwili. 

  1. Hutibu tatizo la ugumba

Ugumba unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi, ingawa imethibitishwa pasipo shaka kwamba mafuta ya habbat soda yamewasaidia wengi kuimarisha afya zao za uzazi. Watu wenye tatizo la uzazi au ugumba wanapaswa kutambua kuwa mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo ya ugumba kwa zaidi ya miaka 2000 sasa. Mpaka leo bado mafuta haya yanaendelea kuripotiwa kuwa ni dawa bora zaidi ya asili kwa ajili ya kurekebisha tatizo la ugumba kwa watu wa jinsia zote.

Wakati huo huo yamethibitika kuwa dawa bora zaidi ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na hutibu tatizo la nguvu za kiume hata kama mwanamume atakuwa na umri wa miaka 120. Unachohitaji ni kuyatumia kwa kipindi kirefu hata miezi miwili au zaidi mfululizo kama tatizo limekuwa sugu. 

  1. Huotesha nywele

Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele. Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kuwa mtumiaji kuliko faida zake. Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upara, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya wanashauriwa kutumia mafuta haya kwa matatizo yote. Ingawa haieleweki ni kwa namna gani yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo na uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake. Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa na huwa mazito kidogo. 

  1. Hutibu mafua na homa

Mafua na homa ni matokeo ya kushuka kwa kinga ya mwili na kadri unavyoendelea kuyavumilia magonjwa kama haya ndivyo unavyozidi kuidhoofisha zaidi kinga ya mwili. Kama tulivyoona kabla kuwa mafuta ya habbat soda huongeza kwa haraka sana kinga ya mwili, huondoa haraka sumu mwilini na bakteria mbalimbali hivyo kufanya kuwa ndiyo dawa nzuri ya asili dhidi ya mafua na homa za mara kwa mara. 

  1. Hutibu majipu

Liwe ni jipu moja au majipu mengi kwa pamoja, mafuta ya habbat soda ndiyo dawa nzuri ya kukupatia nafuu ya haraka. Hii ni kwa sababu kwa sehemu kubwa majipu ni matokeo ya maambukizi ya bakteria na mchafuko wa damu. Mafuta ya habbat soda ni wakala mzuri wa kuondoa bakteria na kusafisha damu na hivyo kuwezesha majipu kuwa chini ya ulinzi. 

  1. Hutibu kikohozi na pumu

Ile sifa yake kuu ya kuondoa vivimbe kwenye tyubu za koo, kitendo chake cha kuongeza kinga ya mwili, kuua bakteria na virusi ndiyo sababu za mafuta haya kutumika kutibu kikohozi na pumu.

Imeandikwa katika historia kuwa mababu wa zamani wa Misri walikuwa wakitumia mafuta ya habbat soda hasa kwa ajili ya kuimarisha afya ya mfumo mzima wa upumuaji.

  1. Hutibu kuharisha

Mara nyingi kuharisha ni matokeo ya maambukizi ya virusi na bacteria, hudhibiti baktria na virusi mbalimbali mwilini na hivyo kufanya ndiyo dawa nzuri mbadala kwa ajili ya kutibu au kuzuia kuharisha.

Huweka sawa mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na tumbo kwa ujumla na hivyo kuzuia mwili wako kupatwa na tatizo la kufunga choo. 

  1. Hutibu shinikizo la juu la damu

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya shinikizo la juu la damu ni moja kati ya matumizi makubwa ya mafuta haya kwa sasa. Ingawa haijathibitishwa rasmi kama dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu lakini wagonjwa wengi wa shinikizo la juu la damu wameripoti kushuka kwa kiwango kikubwa cha mashinikizo yao ya damu wakati wanapotumia mafuta.

Tafiti kama hizi zimesababisha wengi kuanza kutumia mafuta ya habbat soda kama dawa ya asili kwa ajili kutibu shinikizo la juu la damu.

  1. Huondoa tatizo la kukosa usingizi

Tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya asili dhidi ya tatizo la kukosa usingizi na matatizo mengine kama hayo ya kuvuruga utulivu wa usingizi kwa ujumla. Watu wengi wameripoti kupata usingizi mororo na utulivu kwa ujumla baada ya kutumia habbat soda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles