24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

HABARI NJEMA WATAKAOJIFUNGUA SIKUKUU YA PASAKA

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

Serikali imetoa maboksi 40 ya vifaa vya kujifungulia kwa wajawazito watakaojifungua katika kipindi cha Sikukuu ya Pasaka

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo Alhamisi Machi 29, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Grace Maghembe amesema vifaa hivyo vitasambazwa kwenye baadhi ya vituo vya afya na zanahati zilizopo katika Halmashauri tano za mkoa huo ili waweze kupatiwa wajawazito watakaojifungua katika kipindi hicho.

“Lengo la serikali ni kuboresha huduma za afya ikiwamo afya ya mama mjamzito na watoto wachanga wenye umri chini ya miaka mitano, ndiyo maana serikali imetoa vifaa hivi ili kuhakikisha wajawazito wanajifungua salama,” amesema Dk. Maghembe.

Amesema vifaa hivyo vitasambazwa kwa waganga Wakuu wa halmashauri hizo ili waweze kuvipeleka kwenye vituo vilivyotagwa Kwa ajili ya kuvigawa Kwa wahusika.

Alisema Kwa upande wa Kigamboni, vifaa hivyo vitapelekwa kwenye vituo vya Kigamboni, Vijibweni na Temeke vituo vya Temeke wakati Halmashauri ya Ilala watapewa vituo vya Kinyerezi, Kitunda, Pugu na Buguruni.

Katika mgawo huo, amesema kila zahanati itapewa boksi nne ambazo ndani yake kuna vifaa 40 Vya kujifungulia.

“Ukienda kununua kwenye maduka ya dawa, kifaa kimoja kinauzwa zaidi ya 150,000, lakini tumeamua kutoa zawadi Kwa kuwapa vifaa bure wanawake wote watakaaojifungua kipindi cha pasaka,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles