27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Habari njema virusi vya corona

MWANDISHI WETU Na MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA

TANGU uzuke ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona mwezi Desemba mwaka jana nchini China na kisha kusambaa katika nchi kadhaa duniani, kila mmoja amekuwa na hofu hasa kutokana na jinsi ugonjwa huo unavyoambukiza. 

Lakini pamoja na hayo ufuatao ni uchambuzi wa taarifa njema dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo.

Kwanza, hatua ya wataalamu wa afya kufahamu kugundua ndani ya siku 10 ni ugonjwa gani, inatajwa kama mwanzo mzuri dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo tofauti na ilivyokuwa wakati ukimwi ulipoingia.

Inaelezwa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa ukimwi kilitangazwa Juni, 1981 na ilichukua zaidi ya miaka miwili kugundua virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.

Visa vya kwanza vya ugonjwa hatari wa mapafu viliripotiwa nchini Chinamwezi Disemba, 31  2019 na ilipofikia Januari 7 virusi hivyo tayari vilikuwa vimegunduliwa. 

Tayari inajulikana kwamba ni virusi vipya kutoka familia moja na virusi vya SARS . 

Ugonjwa huo umepatiwa jina COVID19 unahusishwa na virusi vya corona kutoka kwa popo.

Jambo la pili, inajulikana jinsi ya kuvigundua katika mwili wa mwanadamu

Lakini jambo la tatu ni kwamba vipimo vilivyoboreshwa ama Sampuli ya RT-PCR inapatikana kila mahali tangu Januari 13.

Hali kadhalika vipimo kadhaa vimefanywa ili kugundua ni nani anayebeba virusi vya corona.

Pamoja na kwamba hali si nzuri kwa nchi kama Italia ambako vifo vya ugonjwa huo vimepanda kwa kasi hadi kufikia 197 jana, nchini China ambako virusi hivyo vilianzia hali inaimarika

Udhibiti mkali na mikakati ya kuwatenga walioambukizwa imezaa matunda.

Kwa wiki kadhaa sasa idadi ya watu wanaopatikana na virusi hivyo imepungua kila siku. Katika mataifa mengine, visa vya maambukizi vinafuatiliwa kwa kina .

Mikakati iliyowekwa ni ya nguvu na visa vinaweza kudhibitiwa kwa urahisi kwa mfano nchini Korea Kusini na Singapore.

Taarifa nyingine njema ni kwamba asilimia 80 ya visa vyote vilivyobainika havijaonyesha makali

Inaelezwa kuwa ugonjwa huo hautoi ishara ama hauna makali kati ya visa asilimia 81.

Katika asilimia 14 iliyosalia vinaweza kusababisha ugonjwa hatari wa mapafu na asilimia tano tu vikiwa hatari na hata kusababisha kifo.

Pamoja na yote hayo, watu wanaopata virusi hivyo wanapona.

Takwimu pekee ambazo zinaripotiwa kwenye vyombo vya habari ni ongezeko la visa vilivyothibitishwa na idadi ya vifo.

Lakini kuna idadi kubwa ya watu walioambukizwa ambao  wamepona. 

Idadi ya watu waliopona ni mara 13 zaidi ya waliofariki na idadi hiyo inazidi kuongezeka.

Pia virusi hivyo haviwaathiri watoto karibia wote.

Ni asilimia tatu pekee ya watu walio chini ya umri wa miaka 20 walioathirika na idadi ya vifo ni asilimia 0.2. kwa watu walio chini ya umri wa miaka 40.

Miongoni mwa watoto dalili ni chache na wakati mwingine hazionekani.

Taarifa za kitaalamu zinaeleza kuwa pia ni rahisi kuua virusi hivyo.

Kwamba vinaweza kuuliwa katika sakafu kwa kutumia  ethanol, Hydrogen peroxide au sodium hypochlorite ndani ya dakika moja pekee.

Ndio maana inasisitizwa juu ya uoshaji wa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji na sabuni kamba hiyo ndio njia bora ya pekee ya kuzuia maambukizi.

Aidha kuna takriban ripoti 150 za kisayansi kuhusu ugonjwa huo.

Katika kipindi cha mwezi mmoja , takriban ripoti 164 zimeandikwa kuhusu ugonjwa COVID19 au SARSCov2, ikiwemo ripoti nyingine nyingi zaidi ambazo hazijachapishwa.

Ripoti hizo zinaandaliwa na watunzi kote duniani.

Kwa kuongezea ni kwamba majarida mengi ya kisayansi yameweka wazi ufadhili wao wa virusi vya corona.

Taarifa inayotia moyo zaidi ni ile ya kuwapo kwa sampuli tofauti za chanjo zinazojaribiwa.

Uwezo wa kutafuta chanjo tofauti ni mzuri. Tayari kuna zaidi ya miradi minane dhidi ya virusi hivyo.

Kuna makundi yalioanzisha juhudi za kutafuta chanjo dhidi ya virusi vingine kama hivyo.

Kinachochukua muda ni  uboreshaji wake, vipimo vyote muhimu vya sumu yake, madhara yake , usalama wake , kinga na uwezo wake katika kinga.

Maabara kadhaa kote duniani zinafanya kazi kuhusu chanjo ya virusi hivyo

Tayari kuna majaribio 80 ya kutafuta tiba ya virusi vya corona.

Hizi ni dawa ambazo zimetumika kwa mambukizi mingine ambayo tayari yamethibitishwa na tunajua ziko salama.

Mojawapo ya dawa hizo ambayo tayari imejaribiwa katika binadamu ni dawa ya remdesivir – dawa ya virusi vya ukimwi ambayo bado inafanyiwa utafiti ambayo imejaribiwa dhidi ya magonjwa kama vile Ebola na SARS/MERS.

Dawa nyingine ni ile aina ya Chloroquine, dawa ya kukabiliana na malaria ambayo pia ina uwezo wa kukabiliana na virusi.

Inajulikana kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi.

Dawa za kukabiliana na virusi zimependekezwa na watafiti kutoka Chuo kikuu cha Ural Federal 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles