26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

GWAJIMA, WASAIDIZI WAKE KUHUKUMIWA JULAI

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima

 

 

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wasaidizi wake watatu wanaotuhumiwa kushindwa kuhifadhi silaha na risasi wanatarajiwa kuhukumiwa Julai 31, mwaka huu.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, baada ya jana wakili wa utetezi, Peter Kibatala kueleza kuwa wamefunga ushahidi wao wa mashahidi sita.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha alisema  anaahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, mwaka huu kwa ajili ya kusoma hukumu.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali, Shedrack Kimaro na Joseph Maugo.

Awali katika kesi hiyo, Muuguzi wa Hospitali ya TMJ   Dar es Salaam, Devotha Bayona na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, George Kiwia, walitoa ushahidi wao.

Shahidi Devotha alidai   yeye ni Ofisa Muuguzi, daraja la pili katika Hospitali ya TMJ na yupo kitengo cha ICU.

Alidai   Machi 29, 2015 aliingia zamu ya usiku katika hospitali hiyo akipokea zamu kutoka kwa muuguzi Rebecca ambaye aliacha kazi mwaka 2016 wakati huo Askofu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo kwa siku ya tatu.

Alidai anakumbuka siku hiyo walifika hospitalini hapo askari wawili na mtu mwingine Bihagaze, wakagonga mlango wa ICU wakihitaji mkoba wa mgonjwa, walivyojitambulisha alitaka kuhakikisha hivyo alimfuata Gwajima na kumuuliza.

Alidai alipomuuliza Gwajima alisema Bihagaze ni msaidizi wake na kwamba Bihagaze alikuwa pamoja na askari hao waliokuwa wanataka mkoba wa mgonjwa.

Muuguzi huyo alidai Gwajima aligoma kutoa mkoba hadi apewe maelezo maalum na kwamba mkoba huo ulikuwa pembeni mwa kitanda cha Gwajima.

Devotha alidai alipopewa majibu hayo aliwaambia polisi kwamba hawezi kulitoa hadi waandike maelezo, wakamueleza wanachohitaji ni mkoba na maelezo wataandika siku inayofuata.

“Polisi walitaka kuingia kwa nguvu nikawaambia hapa ni ICU hamuwezi kuingia kinguvu lakini Gwajima aliniambia kama wanalihitaji kinguvu nichukue mkoba nimpe Bihagaze awape polisi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles