27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

GWAJIMA HANA HATIA, VIGOGO NISHATI WASHTAKIWA KUHUJUMU UCHUMI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu waliokuwa wanakabiliwa na shtaka la kushindwa kutunza silaha.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, amesema mahakama imechukua uamuzi huo baada ya kupitia maelezo ya ushahidi uliotolewa na Pande zote mbili na kubaini kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha pasipo shaka.

“Nimeamua kumuachia huru Gwajima na wenzake watatu katika kesi yao ya kushindwa kutunza silaha kwani ushahidi haukufikia kiwango kinachotakiwa kwani upande wa Jamhuri haujaweza kuthibitisha maelezo ya ushahidi wao,” amesema Hakimu Mkeha.

Askofu Gwajima  alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutohifadhi vizuri silaha huku wenzake  George Mzava, Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Mzava wao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.

Wakati huo huo, mahakama hiyo imewapandisha kizimbani aliyekuwa Mkurugenzi  Mkuu wa tathimini wa Wizara ya Nishati na Madini Archard Karugendo (49) na Mthamini wa madini wa Serikali, Edward Rweyemamu (50), kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara zaidi ya Sh bilioni mbili.

Wakili wa serikali Paul Kafushi akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, amesema washtakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31 mwaka huu maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles