29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Guterres awasihi wapignaji wa Gaza wajizuie

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anafuatilia hali ilivyo katika ghasia zinazoendelea kushika kasi huko ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, kati ya wanamgambo wa kipalestina na Israel, huku akiwa na wasiwasi mkubwa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari ni kwamba wanamgambo wa kipalestina wamerusha makombora 600 ya roketi mwishoni mwa wiki kuelekea upande wa Israel ambapo jeshi la Israel liliingia kati na kwamba waisrael watatu waliuawa ilihali upande wa Gaza watu 15 wameripotiwa kuuawa.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na msemaji wake mjini New York, Marekani, imemnukuu Katibu Mkuu akisema kuwa kinachoendelea kinazidi kuhatarisha hali iliyopo na pia kusababisha vifo vya watu wakati wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Amelaani vikali urushaji wa makombora kutoka Gaza kuelekea Israel hususan ulengaji wa maeneo ya raia.

Katibu Mkuu amesihi pande zote kujizuia na kuacha mara moja mashambulizi na badala yake zifanye maelewano yaliyokuwepo miezi michache iliyopita.

Msemaji huyo wa Katibu Mkuu amesema, mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa Nickolay Mladenov anashirikiana kwa karibu na Misri pamoja na pande husika ili kurejesha utulivu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles