30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Guardiola: Sijaona wa kufanana De Bruyne

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amedai kwa sasa hajaona kiungo duniani wa kumfananisha na staa wake Kevin De Bruyne.

Juzi kiungo huyo alikuwa kwenye ubora wa hali ya juu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya mabingwa Liverpool kwenye Uwanja wa Etihad.

Katika mchezo huo Liverpool ambao wamekuwa kwenye ubora mkubwa msimu huu wakishinda michezo mingi kuliko timu zote England, walikutana na kipigo cha mabao 4-0, ambacho ndio kipogo cha kwanza kikubwa kwa timu hiyo msimu huu wa Ligi Kuu.

De Bruyne alikuwa wa kwanza kuwapatia Manchester City bao katika dakika ya 25 kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Liverpool, Joe Gomez kumchezea vibaya Raheem Sterling ambaye alikuja kuhusika kwenye mabao mawili dhidi ya waajiri wake wa zamani huku mwenyewe akifunga bao dakika yan 35, kabla ya bao la tatu kuwekwa wavuni na Phil Foden baada ya kazi safi iliyofanywa na De Bryune.

Lakini bao la nne liliwekwa wavuni na Alex Oxlade- Chamberlain kwa kujifunga dakika ya 66. Katika mabao hayo manne De Bruyne alihusika kwenye mabao mawili, hivyo kumfanya kocha wake Guardiola kuinuka na kummwagia sifa mchezaji huyo.

“Ni mchezaji mwenye uwezo wa hali ya juu. Ana kitu fulani tofauti na wengine, ana uwezo wa kukimbia, ana mitazamo ndani ya uwanja, anajua kufunga, anapiga pasi za mwisho, ninaweza kusema kwa sasa hakuna mchezaji bora katika safu ya kiungo duniani kama alivyo yeye,” alisema kocha huyo.

Kutokana na hicho anachokifanya mchezaji huyo viongozi na mashabiki wa timu hiyo wanahofu kuja kumkosa staa huyo mwishoni mwa msimu huu.

Wanaamini kikubwa ambacho kinaweza kumfanya mchezaji huyo kuondoka ni Manchester City kushinda kwa rufaa yao ya kufungiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa miaka miwili ambapo rufaa yao itasikilizwa katikati ya mwezi huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles