27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Guardiola atuma salamu Real Madrid

 MANCHESTER, ENGLAND 

BAADA ya timu ya Manchester City kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la FA dhidi ya Arsenal mwishoni mwa wiki iliopita, kocha wa timu hiyo Pep Guardiola, amedai nguvu zao wanazihamishia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Juzi Manchester City walikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Arsenal hatua ya nusu fainali, lakini Guardiola anaamini timu yake itakuja kivingine kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa mwezi ujao. 

Mchezo wa kwanza hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester City iliweza kushinda mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, hivyo mchezo wa marudiano utapigwa Etihad ambapo Manchester City watakuwa nyumbani Agosti 7. 

“Siwezi kuwaambia chochote, lakini najua kwamba wanajua, tunajua ubora tulionao kwa sasa na aina ya wachezaji waliopo, hivyo 

 tutaona nini tulichojifunza au nini tunatakiwa kujifunza. “Kuna baadhi ya michezo haikuwa mizuri kwetu kwa siku za hivi karibuni dhidi ya Bournemouth pamoja na jana (juzi) dhidi ya Arsenal, nadhani tulistahili kupoteza, ila akili yetu kwa sasa ni michezo ya Ligi ya Mabingwa. 

“Ili tuweze kwenda hatua inayofuata wala hapahitajiki miujiza, kikubwa ni kuboresha ubora wetu zaidi ya hapa tulipo, lengo letu ni kuingia hatua inayofuata na ikiwezekana hadi kuchukua ubingwa na sasa tupo tayari,” alisema kocha huyo. 

Februari mwaka huu Manchester City walifungiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu miwili kutokana na kuvunja sheria za matumizi ya fedha michezoni, lakini wiki moja iliopita waliruhusiwa kushiriki kama kawaida kutokana na kushinda rufaa yao, hivyo baada ya kushindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu wamedai wanataka taji la UEFA. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles