27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Guardiola ampigia simu Messi kwa Siri, amshauri asiondoke Barcelona

Lionel_Messi_2205072bPEP Guardola amemshauri mshambuliaji Lionel Messi kubakia Barcelona akimtaka nyota huyo wa Argentina kuwa mtulivu na kuonyesha imani kwa mipango ya kocha wake wa sasa, Luis Enrique.
Wiki iliyopita mchezaji huyo aliyewahi kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka mara nne, aliweka wazi kuwa huenda akaondoka Camp Nou baada ya kukiri kuwa hajui atakuwa wapi msimu ujao.
Mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kumwaga fedha ili kumnasa mchezaji huyo, akidaiwa kutokuwa na furaha baada ya kuwekwa benchi katika mchezo ambao Barca walifungwa bao1-0 dhidi ya Real Sociedad mwanzoni mwa mwezi huu.
Kocha huyo wa Bayern Munich, Guardiola amemwambia Messi awe na shukrani na Barca na kutambua kile ambacho amepewa na klabu hiyo, kuanzia upande wa soka na maisha ya kawaida. Pia Guardiola amemkumbusha nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, aangalie jinsi anavyoungwa na kila mmoja akisema kuwa hakuna klabu nyingine ambayo itakuwa karibu naye kwa kiwango kikubwa kama Barcelona.
Messi amekuwa na desturi ya kuwasikiliza wale ambao anawaheshimu na waliosaidia kipaji chake hasa kocha wake wa zamani, Guardiola ambaye amemsaidia kwa kiwango kikubwa.
Wawili hao walinyakua mataji matatu ya La Liga, mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengine mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia ndani ya misimu minne ambayo Guardiola ameinoa klabu hiyo.
Pep alisisitiza kuwa Luis Enrique anakilakitu cha kumfanya afanikiwe na klabu hiyo ya Catalanna kumtaka Messi awe mvumilivu na kujitoa kwa klabu, akimuahidi kuwa rais ajaye kwenye klabu hiyo atarekebisha mambo yote yaliyokwenda kombo ndani ya miezi 12.
Rais wa zamani wa klabu hiyo Sandro Rosell alilazimishwa kuondoka kufuatia kitendo chake cha kuvujisha siri za usajili za nyota wa Brazil, Neymar.
Ambapo walifungiwa kufanya usajili kwa misimu miwili na FIFA, baada ya kudai wakuvunjasheriazausajiliwawachezajichiniyaumriwamiaka18.
Messi ambaye hana uhusiano wa karibu na kocha wake Luis Enrique wala watu waliomo kwenye bodi ya klabu hiyo, amedaiwa kuupokea ushauri wa kocha wake huyo wa zamani, ambaye alidaiwa kufanya naye mazungumzo ya siri kwa simu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles