21 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Guardiola alalamikia maamuzi ya VAR

MANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya Manchester City kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Tottenham hatua ya robo fainali, kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, amedai mfumo wa VAR umewaangusha.

Mchezo huo ulimalizika kwa Manchester City kushinda mabao 4-3, lakini walishindwa kusonga mbele kutokana na bao 1-0 walilofungwa na Tottenham katika mchezo wa awali, hivyo Manchester City wameshindwa kuendelea kwa kuwa wameruhusu mabao mengi nyumbani kwao japokuwa ni jumla ya mabao 4-4.

Hata hivyo, Manchester City walionekana kuwa na nafasi ya kusonga mbele hatua ya nusu fainali, lakini bao lao katika dakika za lala salama lilikataliwa na mwamuzi kupitia mfumo wa VAR ambapo bao hilo lilikuwa linawapeleka nusu fainali.

Kwa upande mwingine bao la tatu la Tottenham lilionekana kuwa na utata baada ya mchezaji wao, Fernando Llorente, kufunga huku mpira ukianza kumgusa kwenye mkono, lakini mwamuzi alidai ni bao mara baada ya kwenda kujiridhisha kwenye mtambo huo wa VAR, lakini ukiangalia kwa kona mbalimbali, inaonekana kuwa mpira huo ulimgonga kwenye mkono mchezaji huyo.

Kutokana na hali hiyo, Guardiola ameonekana kulalamika huku akidai kwamba mfumo huo wa VAR umekuwa katili kwa upande wao, lakini Tottenham umewabeba.

“Katika dakika 20 za kwanza, matokeo yalikuwa 3-2, hayo ni mabao matano ambayo ni kitu cha kawaida, lakini tumekuja kushangazwa na bao walilofunga wapinzani wetu kwa kutumia mkono lakini VAR wakakubali kuwa bao, wakati huo kwa upande wetu bao la Sterling VAR inakataa na kudai kuwa ni bao la kuotea.

“Nimekuwa nikiisapoti VAR kwa kiasi kikubwa, lakini ukweli ni kwamba bao la Fernando Llorente wameliangalia kwa upande mmoja, inawezekana wameliangalia kwa upande ambao alikuwa mwamuzi,” alisema Guardiola.

Mchezo mwingine ambao ulipigwa juzi ni pamoja na Liverpool ambao walifanikiwa kushinda mabao 4-1 dhidi ya FC Porto na kuwa jumla ya mabao 6-1 baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa ushindi wa mabao 2-0.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles