26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Guardiola: Aguero atabaki kuwa mpiga penalti

Sergio Aguero
Sergio Aguero

MANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa timu ya Manchester City, Sergio Aguero, ameruhusiwa na kocha wake, Pep Guardiola, kuendelea kuwa mpiga penalti muhimu wa timu hiyo.

Kauli hiyo inatokana na nyota huyo kukosa moja ya penalti na kupiga ‘hat trick’ katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa.

Guardiola alisisitiza kwamba licha ya makosa yaliyojitokeza kwa mchezaji huyo, ataendelea kuwa mpigaji muhimu wa penalti katika timu hiyo.

“Ninamwamini Aguero ataendelea kuwa mpigaji wetu muhimu wa penalti.

“Ndiyo, aliwahi kukosa penalti mbili lakini alitamani kuendelea kujaribu nyingine, ninampenda mchezaji wa aina hiyo anayependa kuwajibika.

“Ukweli ni kwamba, kukosa penalti ni moja ya mchezo lakini kitu cha muhimu mhusika asikate tamaa,” alisema Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles