21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Guardiola agoma kurudi Bayern Munich

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amezisikia tetesi zinazomuhusisha na Bayern Munich na ameamua kufunguka,hana sababu ya kuondoka katika klabu hiyo.

Guadiola ametoa kauli hiyo kutokana na minong’onong’ono iliyoibuka kuwa huenda akaikacha timu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuipa mataji mawili ya Ligi Kuu England.

City iko nyuma kwa pointi tisa nyuma ya Liverpool inayoongoza msimamo wa ligi, hali inayozidisha  uvumi juu ya hatma ya Guardiola kwenye kikosi hicho.

Kumekuwa na ripoti zinazomuunganisha na kurudi Bayern Munich ambako alidumu kwa misimu kadhaa akitawala Ligi Kuu Ujerumani.

Mkufunzi huyo wa kiamataifa wa Hispania, amekabaikiza mkataba wa miezi 18 wa kukikonoa kikosi hicho.

Akizungumzia juu tetesi hizo, Guardiola alisema: “Ikiwa watu wanauliza ‘ninataka kukaa?’ Nataka kukaa, sina sababu zozote za kutoka hapa.

“Nimeridhika sana kufanya kazi na klabu hii, na wachezaji hawa.

“Na kama watu wanafikiria nitajiuzulu au kufukuzwa  kwa matokeo haya na ukweli tuko pointi tisa nyuma ya Liverpool basi watu hawanijui.

“Kama klabu inanitaka msimu ujao, nataka kuwa hapa asilimia 100.

Baada ya kupata alama 198 katika misimu miwili iliyopita, City wamejitahidi kupambana kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu.

Lakini, Guardiola anasema atajaribu kupindua kuishusha Liverpool ya Jurgen Klopp na kurudisha timu yake kileleni mwa nmsimamo wa ligi hiyo.

Guardiola aliongezea: “Ninapenda changamoto hii, napenda kuwa katika nafasi hii.

“Ikiwa sitashinda sina shida, najua hivyo. Lakini nimefurahia sana kufanya kazi katika mji huu na kwa klabu hii.

“Na ninataka kusaidia klabu hii kuwa bora.

“Kwanini watu wafikirie kuwa sifurahii hapa? Kwa sababu tulipoteza huko Anfield au nimepoteza michezo mitatu msimu huu?

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles