25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Grumeti Fund yafunda Wasichana 600 Bunda na Serengeti kuhusu kujitambua

Na Malima Lubasha, Serengeti

KAMPUNI ya Grumeti Fund  Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara, kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii ime toa mafunzo kwa wasichana 657 kupitia Program ya Girls Empowerment Session tuko pamoja yaliyole nga juu ya kujitambua, kujisimamia na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike.

Sambamba na hayo pia imetoa taulo za kike kwa wasichana hao kutoka Shule za Sekondari za Hunyari, Sazira na Paul Jones za wilayani Bunda na Sekondari ya Robanda na Mugumu za wilayani Serengeti wata kazotumia kwa mwaka mmoja.

Meneja wa Maendeleo ya Jamii kutoka  Kampuni hiyo ya  Grumeti Fund, Frida Mollel.

Rehema Koka ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mifugo Wilaya ya Serengeti akifungua mafunzo hayo amewasihi wasichana kujisimamia na kutokimbilia mila potofu na kuishukuru kampuni hiyo kuweza kujitoa kuwapa elimu wasichana katika Mkoa wa Mara ikiwemo wilaya ya Serengeti huku akiwasisitiza wasichana hao kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao mbali na kuwepo vikwazo mbalimbali vinavyowazunguka.

“Najua katika kusoma mnapitia changamoto mbalimbali lakini mojawapo ni karo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameitatua na kutatuliwa hiyo zipo changamoto za mila potofu zinazomuathiri mtoto wa kike,hedhi ambayo huwatesa baadhi ya wasichana na kuwapotezea muda kutokana na visumbufu vicha che, lakini pia umbali kwa baadhi ya watoto wa kike pamoja na changamoto ya kukatishwa tamaa,”Alise ma Koka.

Naye, Meneja wa Maendeleo ya Jamii kutoka  Kampuni hiyo ya  Grumeti Fund, Frida Mollel amewataka wasichana hao kujitambua na kujitegemea bila kusubiri watu wengine kuwafanyia maamuzi  ya maisha  yao hasa katika vitu visivyofaa vinavyoharibu maisha yao ya sasa na baadaye .

“Sisi Grumeti Fund  tumekuja hapa kuwapa nguvu na kwamba  wasichana mnahaki  ya kupata elimu,laki ni pia mnahaki ya kusema hapana dhidi ya mila potofu zinazowagandamiza ikiwamo ndoa za utotoni, ukeketaji, mimba za umri mdogo hivyo mnahaki ya kujisimamia na kuachana  na makundi potofu,” amesema Mollel.

Aidha, Mtaalamu wa Afya kutoka Hospitali teule ya Nyerere DDH, Restuta Mruta amewakumbusha wasi chana hao waliohudhuria mafunzo kuwa  wanapoona Hedhi nikiashiria kwamba wako tayari kubeba uja uzito katika umri mdogo kunaweza kupelekea madhara kwa mama na mtoto atakayezaliwa na kuwataka kujikinga kwa mimba za utotokwa kusema hapana lakini pia kuzingatia masomo na hatimaye kutimiza ndoto zao.

Hata hivyo Afisa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Serengeti, Sijali Nyambuche, amewafundisha wasichana hao aina mbalimbali za ukeketaji na kuwakumbusha kuwa mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa inayotekeleza vitendo vya ukekeataji na amewataka kutokubali vitendo hivyo kutokana na madhara makubwa yanayojitokeza kutokana na kukeketwa ambapo aliwahimiza kufika katika maeneo salama ilikutofanyiwa vitendo hivyo.

Nao baadhi ya wasichana waliopata mafunzo hayo  kupitia kongamano hilo wameishukuru Kampuni ya Grumeti Fund kwa kuweza kuwapa elimu hiyo na kuiomba Serikali na wadau wengine kuongeza  zaidi makonga mano ya aina hiyo ili kuelemika zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles