30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Griemann awakataa Platini, Zidane

Antoine Griezman
Antoine Griezman

Paris, Ufaransa

KIUNGO  mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Antoine Griezman  amekataa kufananishwa na wachezaji wakongwe wa timu hiyo, Zinedine Zidane na Michel Platini kwa madai safari yake bado ndefu.

Hatua hiyo imekuja baada mchezaji huyo kuonesha uwezo  mkubwa katika mchezo dhidi ya Ujerumani ambao uliipa timu yake tiketi ya kucheza fainali ya Euro 2016  dhidi ya Ureno.

Katika mchezo huo, Griezmann alifanikiwa kufunga mabao mawili ya ushindi  na kufanya hadi mwisho wa mchezo matokeo yawe  2-0 na kutinga  fainali ya Euro 2016.

“Nina  furaha kwa mafanikio yangu lakini bado nina safari ndefu katika maisha yangu ya soka hadi kuyafikia mafanilio ya Michel Platini ,” maneno ya Antoine Griezmann  wakati akikataa kulinganishwa na nguli huyo wa soka nchini Ufaransa.

Kutokana na rekodi iliyonayo Ufaransa inaamini kwamba huenda wakatwaa kombe hilo katika mchezo utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Stade de France uliopo jiji  la Paris.

Griezmann alisita kukubaliana na ukweli kwamba uwezo wake na juhudi binafsi zinamfanya kuwa miongoni mwa wakongwe  mashuhuri wa taifa hilo.

Uwiano uliopo kati yake na wakongwe hao unatajwa kuwa  chanzo pekee kinachomtambulisha mchezaji huyo bila kuzingatia  timu  anayocheza, aina ya mashindano au mwaka.

Katika Euro  1984, uhodari wa  Platini  wa kusakata  soka ndio ulithibitika baada ya kumaliza akiwa na mabao tisa na kufanikiwa kuwa mfungaji wa michuano hiyo kwa kipindi hicho.

Nyota ya Zidane ilionekana katika Kombe la Dunia mwaka 1998,  baada ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo na kulisaidia taifa lake kunyakuwa kombe hilo.

Mchezo dhidi ya Ujerumani uliofanyika jiji la Marseille, Griezmann alionesha uwezo ambao haukuwahi kuonekana katika kipindi chake alichowahi kucheza soka la kuvutia.

Uwezo huo ndio  unadaiwa kuifanya ngome ya Ujeruamni kuwa dhaifu na kuruhusu adhabu ya penalti  ikiwa  wiki chache tangu akose penalti katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya  Real Madrid.

Hata hivyo nyota huyo ndio mwenye mabao mengi katika michuano hiyo baada ya kufikisha mabao sita na kuongeza uwezekano wa kuendelea kutajwa  zaidi Ufaransa.

Inakumbukwa mchezaji huyo alitoa mchango  muhimu kwa timu yake ya Atletico Madrid na kuiondoa Barcelona katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles