29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

GRAMU 6 ZA ‘COCAINE’ ZAMFIKISHA KORTINI

cocaine-pack

NA BRIGHITER MASAKI (TSJ), DAR ES SALAAM

MKAZI wa Manzese Mvuleni, Justine Jaha (39), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabiliwa na makosa ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya cocaine gramu sita na bangi.

Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Obadia Bwegego, Mwendesha Mashitaka, Faraja Sambala, alidai Juni 16, mwaka jana maeneo ya Manzese Mvuleni alikutwa na madawa hayo anayodaiwa kuyatumia.

“Mtuhumiwa Justine Jaha ukiwa maeneo ya Manzese ulikutwa na madawa ya kulevya gramu 6.9 na siku iliyofuata gramu 6.1 pamoja na bangi huku ukijua kuwa na vitu kama hiyo ni kinyume cha sheria,”alidai Sambala.

Mtuhumiwa alikana kufanya kosa hilo na kuambiwa dhamana ipo wazi ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika ambao watasaini bondi ya Sh milioni tatu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 23, mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo na mtuhumiwa ametoka baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles