Grammy kumpa heshima Nipsey Hussle

0
717

Los Angeles, Marekani

KUELEKEA hafla ya utowaji wa tuzo kubwa duniani za Grammy itakayofanyika mwishoni mwa wiki huko, Los Angeles Marekani, uongozi wa tuzo hizo umetangaza kumpa heshima rapa Nipsey Hussle aliyepoteza maisha kwa kupigwa risasi, Aprili, mwaka jana.

Hafla hiyo itakayofanyika kwenye mji  aliozaliwa Nipsey, umewataja wasanii kama Meek Mill, YG na Roddy Rich kutoa neno kwa rapa huyo anayetajwa kuwa na mchango mkubwa kwa watu wa eneo hilo.

Aidha, rapa huyo anawania vipengele vitatu katika tuzo hizo kama vile Best Rap Song, Best Rap Perfomance na Rap/Sung Performance.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here