25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

GRACA MACHEL AMLILIA WINNIE MANDELA

Na Leah Mushi- GMT – Tanzania


MWANAHARAKATI wa masuala ya wanawake na watoto barani Afrika, Graca Machel, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, Winnie Mandela.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Graca alisema Winnie (81) alikuwa mwanamke shupavu wa kupigiwa mfano na ambaye alihamasisha wengi katika kupigania haki na usawa katika jamii.

“Maisha yake ya ajabu na kipekee yaliyojaa changamoto na harakati yamekuwa kivutio na hamasa kwa watu wengi katika jamii cha kuonesha jinsi ya kujipa moyo, kutokata tamaa pindi tunapokumbwa na changamoto, huku tukiwa na matumaini ya kwamba tutafanikiwa,” alisema Graca.

Alisema Winnie kwake ni dada mkubwa ambaye amekuwa akipendwa wa watu si wa Afrika Kusini pekee, bali duniani kote kwa ujumla kutokana na upendo wake na kujitoa kupigania ukombozi wa taifa hilo.

 

Pamoja na kupita katika kipindi hiki cha machungu na huzuni ya kumpoteza mpendwa wao, Graca amewasihi wote walioguswa na msiba huo kujiimarisha na kuendelea kutetea haki za raia katika jamii zinazowazunguka  kwani kwa kutenda hivyo watakuwa  wakimuenzi Winnie.

 

GRACA MACHEL NI NANI

Graca Machel ni mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto barani Afrika.

Kupitia harakati hizo, amekuwa mwanzilishi wa Wakfu wa Graca Machel (Graca Machel Trust – GMT).

Kupitia wakfu huo, Graca ameweza kuanzisha mtandao wa wanawake Afrika katika masuala ya uwekezaji na uwezeshaji kiuchumi, afya ya mama na mtoto, kilimo biashara na mtandao wa wanahabari.

Graca alikuwa mke wa marehemu Nelson Mandela baada ya kuachana na Winnie (1998- 2013). Makazi yake ni Johannesburg, Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles