GRACA  KUMSHTAKI DAKTARI WA MANDELA

0
395

MAPUTO, MSUMBIJI


MJANE wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Graca Machel, amesema atamshtaki daktari wa Mandela, kutokana na taarifa alizochapisha kwenye kitabu kuhusu siku za mwisho za Mandela.

Daktari huyo, Vejay Ramlakan aliongoza kikosi kilichomhudumia Mandela hadi kifo chake Desemba 2013.

Radio ya Taifa nchini Msumbiji ilitangaza taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Machel ikilaani vikali kitabu hicho.

Graca alisema kitabu hicho kinakiuka heshima ya  Mandela. Kitabu hicho kimeandika taarifa kuhusu siku za mwisho kabla ya kifo cha Mandela.

Miongoni mwa mambo yaliyofichuliwa katika kitabu hicho ni kuharibika kwa gari lililomkimbiza Mandela hospitali, kuchafuka kwa damu na kuingia mapafuni.

Aidha kimetaja kutokuwepo maelewano kati ya madaktari na familia ya Mandela.

Graca anasema kuwa kitabu hicho kilikiuka siri iliyopo kati ya daktari na mgonjwa wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here