GOODLUCK GOZBERT, ANGEL BENARD KUWANIA TUZO KENYA

0
1087

Na CHRISTOPHER MSEKENA


WAIMBAJI wa muziki wa Injili nchini, Angel Benard na Goodluck Gozbert, wamechaguliwa kuwania tuzo za Groove za Kenya, zitakazotolewa Juni 1, mwaka huu nchini humo.

Akizungumza na MTANZANIA, Goodluck alisema amechaguliwa kuwania kipengele cha Mwimbaji Bora wa Mwaka Afrika Mashariki na Kati.

“Muda umebaki mfupi, niwaombe mashabiki wa muziki wangu na Watanzania kwa ujumla wanipigie kura mimi na Angel ili Tanzania tuibuke washindi, kunipigia kura kwa njia ya sms unaandika 26D unatuma kwenda namba 811,” alisema.

Angel Benard yupo kwenye vipengele vitatu, kikiwamo Mwimbaji Bora Afrika Mashariki na Kati, akitumia namba 26D, Wimbo Bora wa Mwaka 5C na Wimbo Bora wa Kushirikiana na namba zake ni 11 D kwenda 811.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here